- Détails
- 591
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuimarisha mazingira ya upatikanaji wa elimu bora kulingana na kasi ya ongezeko la watu Nchini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuimarisha mazingira ya upatikanaji wa elimu bora kulingana na kasi ya ongezeko la watu Nchini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuhakikisha elimu inakuwa miongoni mwa vipaumbele vya mwanzo kwa maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.
Wizara ya elimu na mafunzo ya amali zanzibar imetangaza matokeo ya darasa la nne na darasa la saba na ufaulu umeongezeka kwa asilimia 8.58 ukilinganisha na ufaulu wa asilimia 86.42 wa mwaka 2022.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ya matokeo ya mitihani ya taifa ya darasa la nne na darasa la saba ya mwaka 2023 mkurugenzi wa baraza la mitihani la zanzibar othman omar othman amesema kwa mwaka 2023 matokeo yanaonesha idadi ya watahiniwa 17elfu mia tano na 47 wamefaulu kwa kiwango cha d sawa na asilimia 40.27 ,waliofaulu daraja la c ni asilimia 39.43 , watahiniwa waliopata daraja la b ni asilimia 14.59 na waliopata daraja la a ni asilimia 0.71.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa amefungua Rasmi Hoteli ya SBH Monica Zanzibar ya Kampuni ya ZANPRO Investment Limited, Paje iliyopo Wilaya ya Kusini, Unguja.
Mhe. Lela amesema Serikali ya Awamu ya Nane inayaenzi kwa vitendo Mapinduzi Matukufu ya Mwaka 1964 Kwa kuleta mabadiliko na maendeleo makubwa Kwa wananchi kwa kuwepo kwa miradi mikubwa ambayo inasaidia kuleta ajira kwa wananchi jamboambalo litaweza kubadilisha hali za kiuchumi za wananchi hao na kukuza pato la Serikali Kwa ujumla.
Bank ya NMB imetakiwa kuendelea kuwatunza walimu kwa kuwapa mashirikiano mazuri ya kihuduma pamoja na kutoa masuluhisho mbali mbali ya kifedha.
Amesema hayo Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Abdulgulam Hussein kwa niaba ya Waziri wa Elimu Zanzibar Mhe. Lela Muhammed Mussa, wakati akifungu semina ya siku moja ya shamra shamra za kufikia kilele cha siku ya Waalimu Duniani iliyo fanyika katika ukumbi wa Sheikh Iddrisa Abdul-Wakil Kikwajuni Mjini Unguja .
Amesema, jitahada za Bank ya NMB , ni nzuri na zinaunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Nane chini ya Ungozi wa Rais Mwinyi Katika kuhakikisha wazanzibari waliowengi hasa Waalimu wanajumuishwa katika mfumo rasmi wa kifedha ili kuinua vipato vyao vya kiuchumi.
Amesema, kwa upande wa Bank za akiba na Mikopo, NMB ni miongoni mwa Bank zinazoongoza kwa kubuni bidhaa zinazo lenga mahitaji ya kila makundi ya wateja katika soko hususan waalimu na jamii kwa ujumla.