Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa amefungua Rasmi Hoteli ya SBH Monica Zanzibar ya Kampuni ya ZANPRO Investment Limited, Paje iliyopo Wilaya ya Kusini, Unguja.
Mhe. Lela amesema Serikali ya Awamu ya Nane inayaenzi kwa vitendo Mapinduzi Matukufu ya Mwaka 1964 Kwa kuleta mabadiliko na maendeleo makubwa Kwa wananchi kwa kuwepo kwa miradi mikubwa ambayo inasaidia kuleta ajira kwa wananchi jamboambalo litaweza kubadilisha hali za kiuchumi za wananchi hao na kukuza pato la Serikali Kwa ujumla.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA ndugu Sharif Ali Sharif amesema ujenzi wa Hoteli hiyo yenye hadhi ya Nyota Tano ni mradi uliothibitishwa na Mamlaka ya kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Mwaka 2019 na umegharimu jumla ya Dola za Kimarekani Milioni kumi mpaka kukamilika kwake.
Kwa upande wake Meneja wa Hoteli hiyo Bwana Albert Monsonet ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Kwa mashirikiano waliyoyapata katika kufanikisha mradi huo na ameahidi kufata Sheria zote za Uwekezaji ikiwemo kuwapatia ajira wazawa katika Hoteli hiyo.