THE Revolutionary Government of Zanzibar

Ministry of Education and Vocational Training

Top Management

Hon. Lela Muhamed Mussa

The Minister

Hon. Ali Abdugulam Hussein

Deputy Minister

Mr Khamis Abdulla Said

Principal Secretary

Mr KHALID MASOUD WAZIR

Deputy Principal Secretary Administration

dr. Mwanakhamis Adam Ameir

Deputy Principal Secretary Academic

News & Events

UJUMBE KUTOKA SHANGAI CHINA

Leo tarehe 15/07/2025, Naibu katibu Utawala Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar (WEMA) Ndg Khalid Masoud Wazir na Naibu katibu taaluma Dkt. Mwanakhamis Adam Ameir wamekutana na ujumbe kutoka Shangai-China uliolenga kuimarisha uhusiano na kuwajengea uwezo waalimu wa masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM). Akizungumza na ujumbe huo huko katika ofisi za WEMA Mazizini Naibu katibu Khalid amesema Wizara inashirikiana na wadau mbali mbali ili kuhakikisha kiwango cha Elimu Zanzibar kinaimarika hasa katika masomo hayo. Amefahamisha kuwa lengo kuu la ushirikiano na Shangai ni kuimarisha mipango mkakati ya ufundishaji kwa somo la hisabati ili wanafunzi walipende somo hilo na kukuza kiwango cha ufaulu. Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano (WEMA).

Read More »

MAHAFALI YA KWANZA YA IIT MADRAS – KAMPASI YA ZANZIBAR YAFANA

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Lela Muhamed Mussa, leo amekabidhi vyeti kwa wahitimu wa Shahada ya Pili kutoka Taasisi ya Teknolojia ya India Madras (IIT Madras), Kampasi ya Zanzibar. Mahafali hayo ya kihistoria yamefanyika katika viunga vya kampasi ya IITMZ, yakiwa ni mahafali ya kwanza tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo mwezi Oktoba 2023. Jumla ya wanafunzi 16 wamehitimu masomo yao kwa mwaka wa masomo 2023–2025. Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Elimu, taasisi za elimu ya juu, pamoja na wadau wa elimu kutoka ndani na nje ya nchi. Waziri Lela amewapongeza wahitimu kwa juhudi na uvumilivu wao katika kufanikisha masomo yao, na kuipongeza IIT Madras kwa mchango wake mkubwa katika kuinua kiwango cha elimu ya juu Zanzibar kupitia ushirikiano wa kimataifa. Kampasi ya IITMZ ni matokeo ya ushirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya India, na inalenga kutoa elimu ya kiwango cha juu katika teknolojia na ubunifu kwa vijana wa Zanzibar na kimataifa kwa ujumla. Imeyarishwa naKitengo cha Habari naUhusianoWizara ya Elimu na mafunzo ya AmaliZanzibar .

Read More »

MAAHAFALI YA WALIMU 102 KUHITIMU MAFUNZO YA TEHAMA NA KUKABIDHIWA VYETI YAANDALIWA KATIKA KITUO CHA WALIMU KIEMBESAMAKI

Zanzibar, 17 Juni 2025 – Walimu 102 kutoka skuli 34 zinazohudumiwa na Kituo cha Walimu Kiembesamaki wamehitimu rasmi mafunzo ya matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika ufundishaji na ujifunzaji, katika mahafali yaliyofanyika leo. Mafunzo hayo ya muda wa miezi mitatu yameendeshwa na Idara ya TEHAMA katika Elimu kwa ushirikiano na Kituo cha Walimu Kiembesamaki, yakilenga kuwawezesha walimu kutumia teknolojia kisasa katika kuimarisha mbinu za ufundishaji darasani. Washiriki wa mafunzo hayo walikuwa ni pamoja na Walimu wa Sayansi na Teknolojia, Walimu Wataaluma pamoja na walimu kutoka masomo mbalimbali ya sekondari na msingi. Akizungumza katika hafla hiyo kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu – Taaluma, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Maandalizi na Msingi, Ndugu Ali Mussa, aliwataka walimu hao kuhakikisha wanatumia ujuzi walioupata katika kuinua kiwango cha elimu kupitia matumizi bora ya TEHAMA. Alisisitiza kuwa kwa dunia ya leo inayobadilika kwa kasi kiteknolojia, hakuna nafasi tena ya kufundisha kwa mbinu za kizamani, na hivyo walimu wanapaswa kwenda sambamba na mabadiliko hayo Kwa upande wao, baadhi ya walimu waliohitimu walieleza kufurahishwa kwao na mafunzo hayo, wakisema yamewajengea uwezo mkubwa wa kutumia kompyuta, programu za kielimu, mitandao ya kijamii kwa elimu, na mbinu shirikishi za kidigitali darasani. Mahafali hayo ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika kuimarisha matumizi ya TEHAMA kwenye sekta ya elimu, kwa lengo la kuwaandaa wanafunzi kuwa washindani katika soko la ajira linalozidi kuathiriwa na maendeleo ya teknolojia duniani. Imetolewa na:Kitengo cha Habari na MawasilianoWizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali – ZanzibarTarehe: 17 Juni 2025.

Read More »

WIZARA YAPOKEA UGENI KUTOKA BANK YA DUNIA

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa akiambatana na viongozi mbali mbali wa Wizara hiyo wamepokea ugeni wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania Nathan Balete katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Elimu Mazizini – Unguja. Mkurugenzi wa Benki ya Dunia alipata fursa ya kupokea ripoti ya utekelezaji wa mradi wa kuimarisha ubora wa elimu ya msingi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia iliyowasilishwa na katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ndugu. Khamis Abdullah Said. Imetolewa na Kitengo cha Habari na Uhusino WEMA16/06/ 2025

Read More »

MKUTANO WA NANE WA TATHMINI YA MWAKA YA SEKTA YA ELIMU

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amli Zanzibar (WEMA) Ndg. Khamis Abdalla Said amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Mashirika ya Maendeleo na Asasi za Kiraia katika kuimarisha sekta ya Elimu nchini. Ameeleza hayo wakati akifunga Mkutano wa Nane (8) wa Wadau wa Kutathmini Maendeleo ya Sekta ya Elimu Zanzibar huko Mbweni, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja. Katibu khamis amefahamisha kuwa Mashirika na Taasisi hizo zimekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio yaliyofikiwa sasa katika sekta ya elimu nchini. Amesema Serikali kwa kutambua umuhimu wa sekta ya elimu katika maendeleo ya taifa imewekeza zaidi ili kuhakikisha kunakuwa na wataalamu wa kada mbali mbali, ambapo madarasa 20 ya smart yanatarajiwa kujengwa ili kurahisisha upatikanaji wa elimu na kutatua tatizo la uhaba wa waalimu uliopo hasa katika masomo ya sayansi na hisabati. Nao Washirika wa maendeleo nchini wamesema wataendele kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuimarisha sekta ya elimu Zanzibar.

Read More »

MHE: WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR AIAGA BODI YA AWAMU YA TANO NA KUZINDUA BODI MPYA

Zanzibar, 3 Juni 2025 – Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mheshimiwa Lela Muhammad Mussa, leo ameongoza hafla ya kuwaaga wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya awamu ya tano ya Maamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar, na kuzindua rasmi bodi mpya itakayosimamia shughuli za taasisi hiyo. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa ofisi kuu ya Maamlaka hiyo huko Unguja, na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali, watendaji wa Mamlaka, wajumbe wa bodi wapya na wastaafu na wadau wa elimu ya amali. Akizungumza katika hafla hiyo, Mheshimiwa Lela aliipongeza bodi iliyomaliza muda wake kwa kazi kubwa waliyofanya katika kipindi cha miaka mitatu (Februari 2022 – Februari 2025) katika kuimarisha maendeleo ya Maamlaka hiyo. Amesema mafanikio hayo yamekuwa chachu ya utekelezaji wa sera ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuwawezesha vijana kupitia elimu ya amali. Aidha, Mhe. Lela aliwataka wajumbe wa bodi mpya kufanya kazi kwa mshikamano, weledi na ubunifu katika kusimamia utekelezaji wa mipango ya taasisi hiyo. Alisisitiza umuhimu wa kutumia vyombo vya habari katika kutoa elimu kwa jamii juu ya nafasi ya vyuo vya amali katika kuchochea maendeleo na kupunguza tatizo la ajira. “Mitaala ya elimu inaendelea kufanyiwa mapitio ili kuongeza fani mpya za elimu ya ufundi zitakazowawezesha vijana kupata ujuzi wa vitendo unaohitajika katika soko la ajira na katika kujiajiri,” aliongeza Mheshimiwa Lela. Mapema, Mkurugenzi Mtendaji wa Maamlaka hiyo, Dkt. Bakari Ali Silima, alimkaribisha rasmi Waziri Lela na kuipongeza bodi iliyomaliza muda wake kwa mafanikio makubwa, ikiwa ni pamoja na kusajili vituo vipya 64 vya mafunzo, kuanzisha fani mpya kama vile uvuvi, ufugaji na utalii, pamoja na ongezeko la vijana wanaojiunga na vyuo vya amali visiwani Zanzibar. Kwa upande wake, Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Wakurugenzi, Mhandisi Khamis Adam Khamis, alieleza kuwa bodi hiyo imefanikiwa kutekeleza majukumu yake kwa kiwango kikubwa na kwa kuzingatia sera na vipaumbele vya Serikali. Aliongeza kuwa taasisi hiyo imekuwa nyenzo muhimu katika kuwajengea vijana uwezo wa kujitegemea kiuchumi kupitia mafunzo ya vitendo. Bada ya hotuba hizo, Mwenyekiti mpya wa Bodi, Ndg. Madina Mjaka Mwinyi, ambaye ni Naibu Katibu Taaluma mstaafu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali aliahidi kuendeleza juhudi za maendeleo ya Mamlaka hiyo huku akieleza kuwa changamoto ya rasilimali fedha bado ni kikwazo kwa baadhi ya miradi kufikiwa kwa wakati na katika kipindi chake atajitahidi kuitatua changamoto hiyo. Waziri Lela aliizindua rasmi Bodi mpya ya Wakurugenzi na aliitakia mafanikio katika utekelezaji wa majukumu yake. Hafla ilihitimishwa kwa zoezi la ugawaji wa vyeti na zawadi kwa wajumbe waliomaliza muda wao, ikiwa ni ishara ya kutambua na kuthamini mchango wao mkubwa katika kuiendeleza Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar. Imetolewa na:Kitengo cha Uhusiano – Maamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar.

Read More »

Our Partners