THE Revolutionary Government of Zanzibar

Ministry of Education and Vocational Training

Miradi ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali

Zanzibar Improving Quality of Basic Education (ZIQUE) ni mradi unafadhiliwa na Benki ya Dunia, lengo la Mradi huu unalenga kuboresha ujuzi wa ufundishaji na matokeo ya ujifunzaji, pamoja na kupunguza tofauti ya kijinsia katika viwango vya mpito ndani ya elimu ya lazima. Mradi huu una bajeti ya USD 50 milioni. Mradi huu unatekelezwa kwa miaka saba kuanzia 2023 hadi 2029 na unatekeleza shughuli kama kuimarisha ufanisi wa walimu, kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia kwa kujenga skuli saba za ghorofa Unguja na Pemba, kujenga jengo la Wizara, kufnayia ukarabati vyuo vya ualimu (CCK) Unguja na Pemba na kuziunganisha skuli, vituo vya walimu (TCs) na vituo vya ubunifu wa kisayansi (HUBs) na mkonga wa taifa. Jumla ya USD. 8,314,460.78 zimepatikana na kutumika kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2024/25. 

Skills Development for Youth Employability in the Blue Economy Project (SEBEP) Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano na beni ya maendeleo ya Afrika (AfDB) na Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) una jumla ya UA 38.9 milioni (sawa na USD 54,071,000). Lengo kuu la mradi huu ni Kuwajengea uwezo vijana kwa kuwapatia taaluma zitakazowawezesha kujiajiri au kuajirika ili kuongeza pato la nchi kupitia sekta ya Uchumi wa buluu. Kuimarisha uwezo wa taasisi za maendeleo ya ujuzi kutoa mafunzo ya ubora wa juu na yanayohusiana na soko la ajira, pamoja na kuongeza upatikanaji wa ujuzi wa hali ya juu katika soko la ajira ili kukidhi mahitaji ya viwanda. Itawawezesha vijana kuwa na ujuzi wa kuwafanya waweze kupata ajira katika sekta mbalimbali za Uchumi wa Buluu. Mradi huu unajenga vyuo vya mafunzo ya amali Uguja na Pemba, dakhalia ya wanafunzi wanawake katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Karume (KIST), chuo cha Ubaharia cha SUZA, kutoa mafunzo kwa watendaji wa mamlaka ya mafunzo ya Amali, wakufunzi wa SUZA na KIST.

Global Partnership for Education (GPE III) ni mradi unaofadhiliwa na Global Partnership for Education, ukilenga kuboresha upatikanaji wa elimu bora. Bajeti ya mradi huu ni USD 11,759,000, na unatekeleza shughuli kama kuimarisha ujuzi wa msingi katika kusoma, kuandika, na hesabu, pamoja na kuboresha mifumo ya usimamizi wa walimu.

  1. Uboreshaji wa ujuzi wa msingi katika ngazi ya elimu ya msingi kwa kusisitiza kusoma, kuandika, kuhesabu na ubunifu; Mtaala wa Elimu ya Awali na Msingi unaozingatia Umahiri (CBC) umetosheleza;
  2. Mifumo ya Usimamizi na Maendeleo ya Walimu imeboreshwa;
  3. Uboreshaji wa Usawa wa Kijinsia na Ujumuishaji;
  4. Kuimarishwa kwa Ufanisi na Uadilifu katika Usimamizi wa Elimu;
  5. Uboreshaji wa Mifumo ya Usimamizi na Maendeleo ya Walimu;
  6. Matokeo ya Kujifunza na tathmini zimeimarishwa.

Higher Education for Economic Transformation (HEET) ni mradi unaotekelezwa na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia. Lengo la Maendeleo ya Mradi (PDO) ni kuimarisha mazingira ya ujifunzaji na ulinganifu wa programu na mahitaji ya soko la ajira katika maeneo ya kipaumbele, pamoja na usimamizi wa mfumo wa elimu ya juu. Bajeti ya mradi huu ni USD 20 milioni, na unatekeleza shughuli kama kuboresha ubora wa programu za elimu, kuimarisha miundombinu, na kuongeza matumizi ya teknolojia za kisasa katika elimu.

SIDA inaunga mkono mradi unaolenga kuboresha upatikanaji na ubora wa elimu ya awali na msingi. Mradi huu umepewa bajeti ya SEK 50,000,000, na unatekeleza shughuli zinazohusiana na kuimarisha mifumo ya utoaji elimu na kuhakikisha mazingira ya kujifunza yanafikia viwango vinavyohitajika. Upatikanaji na ubora ulioboreshwa wa Elimu ya Awali na Msingi kwa msisitizo wa kuimarisha mfumo wa utoaji elimu.

  1. Uendeshaji mzuri wa mazingira ya ujifunzaji shuleni kwa kuzisaidia shule kutimiza mahitaji ya msingi;
  2. Kuimarisha taasisi na kujenga uwezo wa Vitengo, Idara, Taasisi na Wakala (UDIAs) wanaotekeleza mradi ili kusimamia Elimu kwa ufanisi na uadilifu;
  3. Kusambaza na kutekeleza Mtaala wa Elimu ya Awali na Msingi unaozingatia Umahiri (CBC).