Wizara ya elimu na mafunzo ya amali zanzibar imetangaza matokeo ya darasa la nne na darasa la saba na ufaulu umeongezeka kwa asilimia 8.58 ukilinganisha na ufaulu wa asilimia 86.42 wa mwaka 2022.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ya matokeo ya mitihani ya taifa ya darasa la nne na darasa la saba ya mwaka 2023 mkurugenzi wa baraza la mitihani la zanzibar othman omar othman amesema kwa mwaka 2023 matokeo yanaonesha idadi ya watahiniwa 17elfu mia tano na 47 wamefaulu kwa kiwango cha d sawa na asilimia 40.27 ,waliofaulu daraja la c ni asilimia 39.43 , watahiniwa waliopata daraja la b ni asilimia 14.59 na waliopata daraja la a ni asilimia 0.71.
Hata hivyo amesema wizara ya elimu inaanda mikakati ya kuchukua jitihada ya kupandisha ufaulu kwa somo la hisabati ambalo bado ufaulu wake ni mdogo.
Amesema watahiniwa 233 wenye mahitaji maalum wamefaulu mtihani huo wakiwemo wasiona wawili ,uoni hafifu 56 ,viziwi 19 ,waemavu wa viungo 12 ,walemavu wa akili 114 na walemavu mchanganyiko ni watahiniwa 30.