Mkurugenzi Idara ya Elimu Mbadala na Watu Wazima Bi Mashavu Abdallah Fakihi amesema Idara itaendelea kufanya jitihada za kuwarejesha katika mfumo rasmi wa Elimu waliotoroka na Waliokosa huduma hiyo.
Bi Mashavu ameyasema hayo wakati Akizungumza na Wazazi pamoja na Wanafunzi wa Elimu Mbadala kwa nyakati tofauti katika Hafla ya Ugawaji wa Vifaa kwa Wanafunzi huko katika Skuli ya Kengeja Wilaya ya Mkoani na Skuli ya Uwandani Wilaya ya Chake Chake ikiwa nishamrashamta za kuelekea kilele Cha Maadhimisho ya Wiki ya Elimu ya Watu Wazima.
Amesema Idara imeshapiga hatua kwa asilimia 90 kupitia Mradi unaofadhiliwa kwa Mashirikiano ya pamoja kati ya UNICEF, Qatar na SMZ wenye Lengo la kuwarejesha Wanafunzi waliotoroka Skuli.
Aidha Bi Mashavu amesema ugawaji wa vifaa utawasaidia Wanafunzi hao kuweza kupata hamasa na hamu yakuendelea na masomo na kujikomboa katika maisha yao ya baadae.