Leo Tarehe 07/09/2023 Watendaji wa Mradi wa sebep (p.a.t) PIT wamekutana na kufanya mazungumzo na Wadau kutoka Katika Taasisi zinazojishuhulisha na Ufuatiliaji wa nishati ya mafuta na gesi nchini, katika ukumbi wa Mikutano Wizara ya Elimu Mazizini Unguja.
Lengo la kikao hicho ni kuhakikisha Mradi huo unapiga hatua kwa kuwashirikisha kila Mdau kwa namna yake.
Kikao hicho kimewashirikisha watendaji kutoka chuo cha Sayansi na Teknolojia Karume (Kist), Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ( zpra) na Wakala wa Kuwawezesha Wananchi Kiuchumi ZEEA.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano (WEMA).