- Détails
- 347
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa amesema, kuwepo kwa Wahandisi Wakike katika nchi kunapelekea kwenda sambamba na Mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia nchini.
Ameyasema hayo wakati wa Ufungaji wa Mkutano wa 8 wa Wahandisi Wanawake, 2023- Uliondaliwa na Taasisi ya Wahandisi, Tanzania Kitengo cha Wanawake, uliyo fanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip Bweni Unguja.
Aidha, amewaomba Wahandisi Wakike kutumia Fursa zinazotolewa na na Serikali. ikiwemo kusajili Makampuni na kujiajiri kupitia Ukandarasi, kwani kufanya hivyo kutasaidia Maendeleo ya nchi kwa Ujumla.
Aidha, ameyapongeza Makundi mbali mbali ya Wahandisi Wanawake kwa Utendaji wao Mzuri, wakiwemo best CEO, best Researcher, best Engineer leader, best Company na best Project. Kwa kupata zawadi inayojulikana kama "Mama Mhandisi Awards".