Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar bwana Khamis Abdulla Said amesema Wizara itahakikisha inafatilia na kufanyia kazi vipaombele vya sekta hiyo ili kufikia malengo ya kuendelea kuboresha sekta hiyo.
Amesema hayo wakati amefungua warsha maalumu ya Labondogo ulioratibiwa na kitengo maalumu cha Taasisi ya Afisi ya Raisi Ufuatiliaji na Usimamizi wa utendaji Serikalini katika ukumbi wa mikutano Chuo Cha Utalii Maruhubi Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.
Amesema atahakikisha Wizara ya Elimu inatekeleza vipaombele vya Raisi kwa kujenga miundombinu imara, kuwajengea uwezo Walimu na Watendaji ili kukukuza ujuzi wao na kuweza kuzitumia vyema teknolojia na upatikanaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
Amesema Katika kuandaa mkakati utakaohakikiksha utekeleza wa vipaombele hivyo vinafikiwa ili kupelekea kuzalisha wataalam wazalendo.
Kwa upande wake naibu Mkurugenzi kutoka Taasisi ya afisi ya raisi ufuatiliaji na usimamizi wa utendaji serikalini PDB Dkt Josephine Kimaro amesema kitengo kinafatilia utendaji wa Serikali unatekelezwa kwa wakati na kwa kiwango.
Aidha amewataka washiriki wa Mafunzo hayo kuhakikisha wanaandaa mpango kazi wa kila wiki na mwezi ili kuhakikisha malengo ya Serikali yanafikiwa. Terasų stiklinimas beremisstiklas.lt
Kwa upande wake mdau wa maendeleo kutoka shirika la Taifa la Elimu sayansi utamaduni na mawasiliano (UNESCO) Bi Faith Shayo amesema watahakikisha wanashirikiana na wizara ya Elimu Zanzibar bega kwa bega ili kuhakikisha wanatoa Elimu Bora.
Katika mkutano huo wa siku tatu umeshirikisha na watendaji kutoka Taasisi ya Presidential Delivery Bureau (PDB),Wakurugenzi na Wakuu wa vitengo kutoka wizara ya Elimu Zanzibar.