Mwanasheria Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Nd. Masudi Mohammed Haji amesema vitendo vya  udhalikishaji vinachangia kwa kiasi kikubwa kurejesha nyuma Maendeleo ya Kimasomo kwa Wanafunzi.

Amesema hayo wakati akifungua Mafunzo ya siku moja dhidi ya udhalilishaji yaliyowashirikisha Wanafunzi wa Skuli ya Uondwe huko katika ukumbi wa Skuli ya Uondwe Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba 

Amesema kutokana na Vitendo hivyo Wanafunzi huathirika kisaikolojia na kupelekea changamoto kubwa kwa maendeleo yao.

Aidha  amesema Mafunzo hayo yanalengo la kuwapa taaluma Wanafunzi hao ili waweze kujilinda na aina mbali mbali za udhalilishaji.

Nae muwezeshaji kutoka kitengo cha sheria Pemba Mw Mohammed Hassan amesema kitengo  kinajukumu la kutoa taaluma dhidi ya udhalilishaji ili Wanafunzi waweze kujitambua. 

Mw Mohammed amesema kuwapatia Mafunzo  Wanafunzi kutawasaidia kujua wajibu wao ili waweze kujilinda na Vitendo hivyo.

Aidha amewataka Wanafunzi kutoa ushirikiano wakutosha kwa Walimu pamoja na Wazazi ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea. 

Kwaupande wake Mw Mkuu wa Skuli hiyo Abdalla Ali Juma amewataka Wanafunzi hao kuyafanyia kazi Mafunzo hayo nakua wawakilishi wazuri katika jamii wanazoishi.