- Détails
- 871
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa amezitaka Taasisi na mashirika yanayotoa elimu ya uzazi na afya kwa wanafunzi wa kike kuwajengea uwezo wa kujitambua na kuepukana na matatizo yanayokwamisha masomo yao.
Akizungumza katika Mkutano wa kutathmini mradi wa kuwajengea uwezo wanafunzi wa ngazi ya Msingi na Sekondari juu kuelewa haki zao na kujua usalama wa afya ya uzazi salama katika maisha yao, Katika ukumbi wa mikutano wa hotel ya Verde huko Mtoni Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.
amesema kufanya hivyo kutaongeza kasi kwa Wanafunzi kujielewa na kujikinga na Mimba za utotoni ambazo zinaathiri maisha yao.