Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar bwana Khamis Abdulla Said amesema kubuni fani mpya zitasaidia kuzalisha wataalam wanaohitajika katika soko la ajira.
Amesema hayo katika hafla ya uzinduzi wa fani mbili mpya fani ya Shahada ya Sayansi ya Maabara Tabibu (bachelor of science in medical laboratory science) na fani ya
shahada ya uzamili ya usimamizi wa biashara na fedha(Master of business administration in finance) katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Cha Taifà SUZA huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema fani hizo zitasaidia kupata wafanyakazi watakaosaidia kutatua changamoto ya vifaa vya afya na kuleta mageuzi ya kiuchumi nchini.
Aidha akizunguzia suala la kufanya tafiti amesema tafiti zitasaidia Sana Serikali kufikia malengo ya kukuza uchumi kwa kujua changamoto na utatuzi wake kutokana na tafiti mbalimbali zitakazofanywa.