Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa Amesema, kuwepo kwa Wafugaji wa Ng'ombe wa maziwa nchini ni msingi mzuri wa kuweza kuimarisha afya kwa jamii.
Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya uhamasishaji wa unywaji wa maziwa kwa wananchi na watoto maskulini na majumbani, iliyo fanyika katika Viwanja vya Nane nane Dole Wilaya ya Magharib "A"Unguja.
Amesema, upo umuhimu mkubwa wa kunywa maziwa kwa binadamu hasa Watoto kwani watajengeka kiakili na kupelekea kufanya vizuri katika Masomo yao.
Aidha, amewaomba wazazi na walezi kuwapatia watoto maziwa angalau Lita Moja kwa Wiki kwani kufanya hivyo kutapunguza Madhara yanayotokana na upungufu wa unywaji wa maziwa ikiwemo udumafu(Mulnutrition) pamoja na upungufu wa Damu mwilini.
Amesema, suala la maziwa kupata doko la uhakika la maziwa , Tayari limeshapatiwa ufumbuzi kwani Jumuiya kupitia Mashirika yake Tanzu ya UDACU NA PDCU itaanza kuchakata maziwa kupitia Kiwanda kidogo kitakacho anza Fuoni na Pemba Chake Chake.
Sambamba na hayo, Waziri Lela amewaomba Watendaji wa Wizara ya Elimu kuimarisha Maabara za Uchunguzi wa Maradhi na Wadudu ili Watoa huduma za Matibabu wawe na Urahisi wa Matibabu kwa wafugaji.
Mapema Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Mifugo Zanzibar, Bw. Sefu Shaaban amesema, Wizara ya kilimo tayari imeimarisha Mashirikiano ya kisheria na Wizara ya Elimu ili kuweza kutatuta changamoto ya Kiwanda cha Chakula cha Mifungo ili kuweza kuimarisha Shughuli bora za Ufugaji.
Amesema, Taifa lazima lijitahidi kuzalisha Rasilimali watu ambao watakuwa ni Msingi Bora wa kulisadia Taifa kwa Ujumla.
Akisoma Risala Katibu wa jumiya hiyo Bi. Asha Mshimba Jecha. amesema, jumuiya ya Wafugaji imeanzishwa mwaka 2021, kwa Mashirikiano na Wanachama Wazilishi 450 wafugaji ng'ombe ambao wanawake 105 na Wanaume 345 Unguja na Pemba.
Amesema, Lengo la kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ni kuwaweka Wafugaji wote katika kitu kimoja ili kukuza Maendeleo ya nchi.
Kauli mbiu ya Maadhimisho hayo inasema "Maziwa safi na salama ni Bora kwa Afya Yetu."
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano (WEMA)
Tarehe : 5/08/2023