Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa amesema, Serikali imedhamiria kuweka mazingira bora ya elimu kwa ngazi zote ili kuleta maendeleo ya Kielimu nchini.
Ameyasema hayo wakati akifunga Maonyesho ya Nne ya wiki ya Elimu ya Juu, yaliyo fanyika katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja.
Ameseama, Maonyesho hayo ni fursa kwa wazazi na wanafunzi katika kuendelea na elimu ya Vyuo Vikuu.
Amesema, wanafunzi ni vyema kutumia fursa hiyo adhimu ya kupata kujiunga na Vyuo Vikuu kwa kwa urahisi ili kuweza kusonga mbele kielimu.
Mapema Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Khamis Abdulla Said amesema, Idadi ya Wanafunzi walofaidika kujiunga na Vyuo Vikuu kupitia Maonesho hayo ni kubwa, jambo ambalo limesaidia sana kupunguza gharama za kutafuta tarifa za Vyuo husika.
Aidha, amewashukuru washiriki wote kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kwa Ushiriki kwao, kwani kumeleta hamasa kubwa kwa Wanafunzi mbalimbali wanaotaka kujiunga na ngazi ya Vyuo Vikuu.
Kwa Upande wao Wadau wa Elimu waloshiriki katika Maonesho hayo, wameishukuru Wizara kupitia kitengo cha Urajis wa Elimu ya Juu Kwa kuandaa maonesho hayo kwani imekuwa ni njia moja ya kuleta muamko na uelewa mzuri kwa Wanafunzi
Kauli mbiu ya Maonesho hayo "Wakufunzi na Wabunifu ni Uti wa mgongo"
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano (WEMA)
Tarehe:5/08/2023