Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar bwana Khamis Abdulla Said amesema kubuni fani mpya zitasaidia kuzalisha  wataalam wanaohitajika katika soko la ajira.


Amesema hayo katika  hafla ya uzinduzi wa  fani mbili mpya fani ya Shahada ya Sayansi ya Maabara Tabibu (bachelor of science in medical laboratory science) na fani ya 
shahada ya uzamili ya usimamizi wa biashara na fedha(Master of business administration in finance) katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Cha Taifà SUZA huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema fani hizo zitasaidia kupata wafanyakazi watakaosaidia kutatua changamoto ya vifaa vya afya  na kuleta mageuzi ya kiuchumi nchini.


Aidha akizunguzia suala la kufanya tafiti amesema tafiti zitasaidia Sana   Serikali  kufikia malengo ya kukuza uchumi kwa kujua changamoto na utatuzi wake kutokana na tafiti mbalimbali zitakazofanywa.

Pia amewasisitiza Wanafunzi wanaojiunga na vyuo  kwa kuangalia fani ambazo zinauhitaji Mkubwa katika soko la ajira  hivyo fani hizo ni vyema Wanafunzi kuzitumia kwani Taifa linauhitaji wa wataalam wa fani hizo.


Kwa upande wake Makamu Mkuu wa chuo cha taifà (SUZA) Profesa. Mohamed Makame  Haji amesèma kuanzisha fani hizo ni kuhakikisha wanaisaidia Serikali  kupata wataalam  wazalendo  watakaoendelea  kuinia uchumi wa Taifa.


Nae naibu makamo Mkuu wa chuo  cha Suza Dkt Ali Makame Usi akitoa maelezo mafupi ya kuanzisha program amesema ni lazma upite hàtua zote hadi ipatikane mtaala kwa ajili ya kufundishia hiyo fani husika


Uanzishaji wa fani hizo mbili zitasaidia  Serikali kupunguza gharama ya ya kusomesha Wanafunzi nje ya Nchi na kupelekea  kuzalisha  wataalam watakaoleta  mafanikio ya utekelezaji mzur na kufikia malengo ya uchumi wa buluu.