Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Ali Abdulgulam Hussein amesema atahakikisha anafuatilia miradi yote iliyopo chini ya Wizara ya Elimu ili ipatikane kwa wakati.
Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi inayoendelea katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema ili miradi ipatikane kwa wakati ni lazima kuwepo kwa mashirikiano baina ya Wizara na Wakandarasi waliopewa miradi hiyo sambamba na ufuatiliaji wa mara kwa mara ili kuweza kuskiliza na kuzipatia ufumbuzi wa haraka changamoto mbalimbali zinazijitokeza katika miradi hiyo.