Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe Suleiman Massoud Makame ameipongeza Wizara ya Elimu Zanzibar kwa kuanzisha maonesho ya Wiki  ya Elimu ya Juu.

Amesema hayo wakati alipotembelea mabanda mbalimbali Katika maonesho ya 4 ya wiki ya Elimu ya Juu Maisara Unguja. 

Amesema maonesho hayo yatasaidia jamii kuweza kutambua chuo na usahihi wake,na fani zinazotolewa.

 Aidha amewataka Wanafunzi kujitokeza kwa wingi  Katika maonesho hayo ili kujua fursa mbalimbali zinazopewa kipaombele katika soko la ajira duniani.