Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa amesema, Kuoengezeka kwa kiwango cha ufaulu Zanzibar kutapelekea Kupiga hatua nzuri ya Kimaendeleo nchini.

Ameyasema hayo wakati wa hafla ya kuwapongeza Walimu wa Kidato cha Sita kwa upande wa Unguja kwa Matokeo mazuri ya mwaka 2022/2023. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari Lumumba Mjini Unguja.

Amesema, ufaulu wa Kidato cha Sita umeongozeka kwa kiasi kikubwa jambo ambalo litapelekea kupatikana kwa Wataalamu bora nchini.

Aidha amesema, Walimu bado wanakazi kubwa ya kuleta Mageuzi katika Sekta ya  Elimu yenye kumlenga Mtoto katika kupata Elimu Bora itakayomsaidia katika maisha yake ya baadae.

Amesema, Wizara inatambua uwepo  changamoto ya Maabara kwa wanafunzi wa Sayansi. Hata hivyo Serikali inajitahidi kujenga Maabara za kisasa kuanzia ngazi ya Msingi hadi Sekondari ili kuleta ufaulu mzuri wa wanafunzi katika masomo hayo.


Mapema Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndugu. Khamis Abdullah  Said amesema, Walimu lazima wahakikishe wanasimamia misingi ya kazi yao ili kuweza kuleta matokeo mazuri zaid.

Amesema, pia Walimu wanajukumu la kuwaandaa Wanafunzi ili kuweza kupata maisha bora yatayowasaidia katika kutimiza Malengo yao ya baadae.

Akisoma Risala Mkurugenzi Idara ya Elimu Sekondari Wizara ya Elimu Zanzibar Bi. Asya Iddi Issa amesema, jumla ya wanafunzi 2587 walifanya Mtihani wa kidato cha Sita.  wanaume 1278 na wanawake 1309 kutoka katika Skuli 41 Unguja na Pemba ikiwa Skuli 27 Unguja na 14 Pemba.

Amesema, Wanafunzi 673 wamepata daraja la kwanza, 1240 wamepata daraja la pili, 657 wamepata daraja la tatu, 15 wamepata daraja nne na Wanafunzi Wawili wamepata Sifuri.

Amesema, Upatikanaji wa matokeo mazuri ya Mwaka 2023 yanatokana na jitihada nzuri za Wizara, Walimu, wanasiasa, Wazazi pamoja na Wadau mbali mbali Walimu.

Amesema, Kutokana na Idadi kubwa ya ongezo la ufaulu , Hivyo ameiomba Wizara kuongeza Skuli Maalum zitakazo weza kupokea wanafunzi ili kurahisisha uwepo wa nafasi za kutosha na upangaji Mzuri wa Walimu.

Kwa upande wao Walimu wa Kidato cha Tano na Sita, Wameupongeza Uongozi wa Wizara ya Elimu kwa Mashirikiano mazuri pamoja na usimamizi mzuri hadi kufanikisha  kufuta ziro kwa Skuli za Zanzibar.

Wamesema, Wizara iendelee na uhamasishaji kwa walimu na wanafunzi pamoja na kupatiwa walimu nyenzo mabali mabli za kufundishia ikiwemo Vitabu ili kuweza kupiga hatua nzuri ya Elimu.

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano (WEMA).
Tarehe:13/08/2023