Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh Leila Muhamed Mussa amesema wanathamini mchango mkubwa unaotolewa na Shirika la Maendeleo la UNISEF katika kutatua suala la maji katika Skuli za Zanzibar. 

Akizindua kitabu cha tathmini ya gharama za huduma ya Maji, ujenzi wa Vyoo na elimu ya afya ya mazingira katika Skuli hafla iliofanyika  katika ukumbi wa Madinatul Bahari Mbweni amesema mpango huo utaleta matukio mazuri kwa wanafunzi katika kujifunzia. 

Amesema  hatua hiyo  italeta matumaini ya kuondosha ongezeko la maradhi mbali mbali pamoja na wanafunzi kupelekea kuwa na mazingira wezeshi ya kuweza kujifunza na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi hao. 

Hata hivyo Mh Leila amewaonba  wadau mbali mbali kuendele kuisaidia Zanzibar katika kutatua suala la vyoo na maji kwani licha ya jitihada zinazochukuliwa bado lipo katika Skuli zinazo wazunguka 

Nae Mkuu wa mpango wa Maji safi na mazingira Tanzania  Frank Odhiambo na kiongozi Mkuu wa Unisef upande wa Zanzibar Laxmi Bhawani wamesema tafiti zilizofanywa  Zanzibar hivi karibuni zinaonyesha kuwa wanawake wengi waliotokea katika mradi wa kufundisha wanafunzi juu ya kutumia maji na kujikinga na maradhi mbali mbali wamepata ajira na uzalishaji  wao kipato umeongezeka.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzi ya Amali  Khamis Abdallah  Saidi amesema lengo la kuanzisha kwa mradi huo ni kuimarisha kwa Skuli zote za Serekali na Binafsi kuishi na kusoma katika mazingira mazuri na salama. TiktokFollowerKaufen.de TikTok Likes Kaufen Mit PayPal

Mradi wa kuwafundundisha wanafunzi juu ya kutumia maji na kujikinga na maradhi umeanzishwa mwaka ...... Na kufadhiliwa Shirika la Maendeleo la Unisef.