
- Details
- 68
Mwanasheria Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Nd. Masudi Mohammed Haji amesema vitendo vya udhalikishaji vinachangia kwa kiasi kikubwa kurejesha nyuma Maendeleo ya Kimasomo kwa Wanafunzi.
Amesema hayo wakati akifungua Mafunzo ya siku moja dhidi ya udhalilishaji yaliyowashirikisha Wanafunzi wa Skuli ya Uondwe huko katika ukumbi wa Skuli ya Uondwe Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba
Amesema kutokana na Vitendo hivyo Wanafunzi huathirika kisaikolojia na kupelekea changamoto kubwa kwa maendeleo yao.