![](/images/WhatsApp%20Image%202023-09-23%20at%203.20.50%20PM.jpg)
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, amewataka wazazi na walezi nchini kuendelea kuwaruhusu vijana wao kushiriki katika michezo, ili kuimarisha ufahamu katika mafunzo yao.
Amesema iwapo wanafunzi watashiriki kikamilifu katika michezo wataweza kuongeza mbinu na kujiamini pamoja na kuimarisha akili zao wakati wa mafunzo.
Makamu wa Pili wa Rais ameeleza hayo wakati wa Kilele cha Tamasha la 59 la Elimu Bila Malipo 2023, hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Skuli ya Sekondari Fidel Castro.
Aidha amewasihi wanafunzi hao kulinda na kuendeleza mila na silka za wazanzibari, wakati wote wanapokua katika michezo sambamba na kudumisha amani.