![](/images/WhatsApp%20Image%202023-09-02%20at%207.00.22%20AM.jpg)
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Nd. Khamis Abdullah Said amesema Kufanyika kwa Maonesho ya Wiki ya Elimu ya Juu Kisiwani Pemba Kuna lengo la kuwasogezea Wanafunzi huduma kwa ukaribu ili waweze kufanya maamuzi sahihi ya Kimasomo.
Ameyasema hayo wakati akifunga Wiki ya Maonesho ya Elimu ya Juu huko katika Uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.
Amewataka Wanafunzi pamoja na Wazazi kuyafanyia kazi maelekezo waliyoyapata kutoka Vyuo mbali mbali kabla ya kutoa maamuzi yao.
Akizungumzia jitihada za Serikali katika kuwapatia Wanafunzi fursa za kujiendeleza kielimu Katibu Mkuu amesema Serikali inafanya utaratibu wa kubadilisha sheria ya Bodi ya Mikopo Zanzibar ili huduma zao ziweze kupatikana hadi ngazi ya Stashahada.
Akifafanua zaidi Nd. Said amesema Serekali zote mbili ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania na Serekali ya Mapinduzi Zanzibar kwasasa zinatoa huduma ya mikopo ili kujiendeleza kuanzia Ngazi ya Shahada.