Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa amefungua Rasmi Hoteli ya SBH Monica Zanzibar ya Kampuni ya ZANPRO Investment Limited, Paje iliyopo Wilaya ya Kusini, Unguja.
Mhe. Lela amesema Serikali ya Awamu ya Nane inayaenzi kwa vitendo Mapinduzi Matukufu ya Mwaka 1964 Kwa kuleta mabadiliko na maendeleo makubwa Kwa wananchi kwa kuwepo kwa miradi mikubwa ambayo inasaidia kuleta ajira kwa wananchi jamboambalo litaweza kubadilisha hali za kiuchumi za wananchi hao na kukuza pato la Serikali Kwa ujumla.