Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Abdulgulam Hussein, amewataka walimu wa Skuli za Mkoa wa Kusini Unguja kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kujikita zaidi katika kuimarisha elimu kwa wanafunzi ili kutoa matokeo mazuri zaid.
Akizugumza katika mafunzo ya siku nne yaliyoandaliwa na taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation MIF yaliyofanyika katika ukumbi wa TC Dubga Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema, walimu ndio wanaowafanya wanafunzi kuleta matokeo bora pindi wakitoa elimu inayostahiki kwa wanafunzi wao, hivyo kupatiwa mafunzo hayo itasaidia kujua mbinu za kujibu mitihani kwa wanafunzi na kuengezeka ufaulu kwa wanafunzi wao.