![](/images/WhatsApp%20Image%202023-08-02%20at%2010.49.19%20AM.jpg)
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Ali Abdulgulam Hussein amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuhakikisha sekta ya Elimu inaendelea kupiga hàtua.
Amesema hayo wakati wa hafla ya Ugawaji wa vifaa vya maabara kwa Skuli ya Sekondari Jongowe Wilaya ndogo Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema Serikali ya awamu ya nane imekusudia kuboresha miundombinu ya Skuli na upatikanaji wa vifaa vya kufundishia ili taifa lizalishe wataalam wazalendo.
Aidha amesema upatikanaji wa vifaa vya kufundishia vitaleta ufanisi katika kukuza kiwango cha ufaulu nchini.