Leo Tarehe 25/09/2023
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Nd. Khamis Abdullah Said amewataka Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Kojani kusoma kwa bidii ili waweze kufaulu kwa viwango vya juu.

Nasaha hizo amezitoa wakati alipotembelea Skuli ya Sekondari Kojani na Kuangalia harakati za Ufundishaji na ujifunzaji katika Skuli hiyo.

Amewataka Wanafunzi hao kudumisha nidhamu ili waweze kufanikiwa katika kufikia malengo waliyojiwekea katika Maisha yao.

Aidha amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejenga Skuli ya kisasa katika kisiwa Cha kojani ili Wanafunzi waweze kusoma katika mazingira mazuri.

Aidha amesema Wizara ya Elimu inatarajia kuanzisha somo la uvuvi katika Skuli ya kojani ili kuwaandaa Wanafunzi katika fani inayoensana na mazingira yao.

Mwalimu Mkuu Skuli ya Sekondari Kojani Nd. Khamis Amour Khamis amesema ziara hiyo ya Katibu Mkuu katika Skuli yake imekuja katika wakati muafaka kuelekea Mitihani ya Kitaifa hivyo itaongeza Ari na hamasa kwa Wanafunzi katika kujiandaa na Mitihani hiyo.

Amesema katika Mitihani ya majaribio kiwilaya ni Wanafunzi 5 tu ambao walipata divisheni zero hivyo ziara hiyo itasaidia kuamsha Ari ya kufuta zero hizo,

Kwa Upande wao Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Kojani wamesema Wamefarijika Sana baada ya kupokea nasaha za Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Wameahidi kuongeza jitihada katika kujiandaa na Mitihani.