• EMIS
  • E-OFFICE
  • Home
  • About Us
  • News and Events
  • Staff Mail
  • Contact Us
  1. You are here:  
  2. Home
  3. News and Events

MOEVT NEWS&EVENTS

KIKAO CHA WATENDAJI WA MRADI WA SEBEP (P.A.T) PIT

Details
11 September 2023
64

Leo Tarehe 07/09/2023 Watendaji wa Mradi wa sebep (p.a.t) PIT wamekutana na kufanya mazungumzo na Wadau kutoka Katika Taasisi zinazojishuhulisha na Ufuatiliaji wa nishati ya mafuta na gesi nchini, katika ukumbi wa Mikutano Wizara ya Elimu Mazizini Unguja.

Lengo la kikao hicho ni kuhakikisha Mradi huo unapiga hatua kwa kuwashirikisha  kila Mdau kwa namna yake.


Kikao hicho  kimewashirikisha watendaji kutoka chuo cha Sayansi na Teknolojia Karume (Kist), Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ( zpra) na Wakala wa Kuwawezesha Wananchi Kiuchumi ZEEA.

 

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano (WEMA).

UTIAJI SAINI MoU YA KUENDESHA MAFUNZO YA GROUND HANDLING KIST.

Details
11 September 2023
47

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imesema, inaunga mkono mpango ulioandaliwa na Taasisi ya  Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), katika utowaji wa mafunzo ya huduma za ndege katika Viwanja vya Ndege.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bw.Khamis Abdalla Said, amesema hayo alipokuwa katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya utowaji wa mafunzo hayo kwa Taasisi ya Karume  na Wataalamu wa huduma za ndege katika viwanja vya ndege, hafla ilifanyika katika  Ukumbi wa Mkutano wa Dkt. Idrissa Muslim Hijja Bweni Zanzibar.


Amesema, hatua hiyo inakwenda sambamba na dhamira ya Serikali juu ya kuimarisha usafiri wa anga hapa nchini.

Amesema, kuwepo kwa mafunzo hayo itachochea kupatikana Wafanyakazi wa kutosha wenye utaalamu wa kutoa huduma kwa kiwango kinachohitajika.

Aidha, Bw.Said amefahamisha kuwa, Vijana wengi wanamaliza elimu zao na kubakia mitaani kufanya mambo yasiostahiki hivyo, kuwepo kwa mafunzo hayo itakuwa chachu ya kutimiza ndoto zao na kuipunguzia mzigo Serikali.

Read more …

MAFUNZO YA URATIBU WA WAZI WA KUPIMA UTENDAJI KAZI WA WATUMISHI

Details
11 September 2023
47

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar bwana Khamis Abdulla Said amesema ili kufikia  malengo ya sekta ya Elimu ipo haja ya kuendelea kuwajengewa uwezo watendaji mbalimbali kwanzia viongozi hadi wanaowasimamia.

 

Amesema hayo wakati wa kufungua Mafunzo ya Uratibu wa wazi wa kupima utendaji kazi wa watumishi katika  ukumbi wa mikutano wa chuo cha Utalii Maruhubi Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.


Amesema kuwepo kwa Mafunzo husaidia kufikia malengo ya taasisi husika kwa wakati. Amewataka washiriki hayo kuitumia  vyema fursa hiyo na kuyafata kwa  vitendo ili kufikia malengo ya taasisi zao.

Read more …

HAFLA YA UGAWAJI WA VIFAA KWA WANAFUNZI KATIKA SKULI YA KENGEJA, PEMBA

Details
11 September 2023
19

Mkurugenzi Idara ya Elimu Mbadala na Watu Wazima Bi Mashavu Abdallah Fakihi amesema Idara itaendelea kufanya jitihada za kuwarejesha katika mfumo rasmi wa Elimu waliotoroka na Waliokosa huduma hiyo.

Bi Mashavu ameyasema hayo wakati Akizungumza na Wazazi pamoja na Wanafunzi wa Elimu Mbadala kwa nyakati tofauti katika Hafla ya Ugawaji wa Vifaa kwa Wanafunzi huko katika Skuli ya Kengeja Wilaya ya Mkoani  na Skuli ya Uwandani Wilaya ya Chake Chake ikiwa nishamrashamta za kuelekea kilele Cha Maadhimisho ya Wiki ya Elimu ya Watu Wazima.

Amesema Idara imeshapiga hatua kwa asilimia 90 kupitia Mradi unaofadhiliwa kwa Mashirikiano ya pamoja kati ya UNICEF, Qatar na SMZ wenye Lengo la kuwarejesha Wanafunzi waliotoroka Skuli.

Aidha Bi Mashavu amesema  ugawaji wa vifaa utawasaidia Wanafunzi hao kuweza kupata hamasa na hamu yakuendelea na masomo na kujikomboa katika maisha yao ya baadae.

Read more …

UFUNGAJI WA WIKI YA MAONESHO YA ELIMU YA JUU HUKO KATIKA UWANJA WA GOMBANI, PEMBA.

Details
05 September 2023
52

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Nd. Khamis Abdullah Said amesema Kufanyika kwa Maonesho ya Wiki ya Elimu ya Juu Kisiwani Pemba Kuna lengo la kuwasogezea Wanafunzi huduma kwa ukaribu ili waweze kufanya maamuzi sahihi ya Kimasomo.

Ameyasema hayo wakati akifunga Wiki ya Maonesho ya Elimu ya Juu huko katika Uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.

Amewataka Wanafunzi  pamoja na Wazazi kuyafanyia kazi maelekezo waliyoyapata kutoka  Vyuo mbali mbali  kabla ya kutoa maamuzi yao.

Akizungumzia jitihada za Serikali katika kuwapatia Wanafunzi fursa za kujiendeleza kielimu Katibu Mkuu amesema Serikali inafanya utaratibu wa kubadilisha sheria ya Bodi ya Mikopo Zanzibar ili huduma zao ziweze kupatikana hadi ngazi ya Stashahada.

Akifafanua zaidi Nd. Said amesema  Serekali zote mbili ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania na Serekali ya Mapinduzi Zanzibar kwasasa zinatoa huduma ya mikopo ili kujiendeleza kuanzia Ngazi ya Shahada.

Read more …

Page 3 of 12

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10

Contact Details

P.O.Box 394 Mazizini, Zanzibar
+255 24 223 2827
info@moez.go.tz

Main Menu

  • Home
  • About Us
  • News and Events
  • Staff Mail
  • Contact Us

Get in Touch

P.O.Box 394 Mazizini, Zanzibar
info@moez.go.tz

Our Institute

  • Kwarara Media Education Centre (KMEC)
  • The State University of Zanzibar (SUZA)
  • Vocational Training Authority(VTA)
  • Zanzibar Higher Education Loan Board(ZHELB)
  • Karume Institute of Science and Technology(KIST)
  • Zanzibar Examination Council(ZEC)
  • Zanzibar Institute of Education(ZIE)

External Links

  • Ministry of Education, Science and Technology (MOE)
  • The National Examination Council of Tanzania (NECTA)
  • The National Council for Technical Education (NACTE)
  • Tanzania Commission for University (TCU)
© MoEVT. Designed by ICT-Department.