Mhe.Lela Muhamed Mussa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar amesema , Wizara itaendelea kushirikiana na Wadau mbali mbali wa Elimu ili kuleta maendeleo bora  katika sekta hiyo.


Amesema hayo wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Upishi Salama wa kutumia Gesi katika  Skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame iliyoko Mkoa wa Kusini Unguja.


Amesema, Wadau wa Elimu kwa kushirikiana na Serikali huleta mabadiliko chanya kwa wanafunzi yatakayo weza kuwasaidia baadae.

Pia Waziri lela ameishukuru Taasisi hiyo na kutoa  wito  kwa  wadau mbali mbali wa Elimu kushirikiana pamoja katika kuunga mkono juhudi  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha  utunzaji wa mazingira unafikiwa lengo.

  
Kwaupande wake Mwenye kiti wa Taasisi ya Mwanamke Intiative Foundation Mhe . Wanu Hafidh Ameir , amesema lengo la Taasisi hiyo ni  kutokomeza   umasikini na maradhi katika uwekaji wa mazingira yaliyo bora katika upatikanaji wa Elimu kwa
kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira  mazuri kwa kuacha kwenda kutafutafuta kuni pamoja na kuwaweka wapishi katika mazingira salama.

Amesema, Programu hiyo ya Upishi Salama imelenga kuzifikia  Skuli 35  kwa Mkoa mzima wa Kusini Unguja.

Akitoa neno la shukrani Msaidizi Mwalimu Mkuu Ndugu Issa Ameir . Ameishukuru Taasisi hiyo kwa kuandaa programu hiyo na kuwapatia majiko ya gesi na ameahidi  kuyatumia vyema ili lengo liweze kufikiwa.

Katika kuendeleza Program ya upishi salama kauli mbiu ni Upishi Salama uwe chachu ya mabadiliko "