
Naibu Spika wa Wabaraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Mgeni Hassan Juma amesema, Ushirikiano ni njia moja ya kuleta Mabadiliko ya Kimaendeleo Nchini .
Ameyasema hayo kwa Niaba ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid wakati akifungua Mkuatano wa Wadau wa Elimu na Kamati ya Ustawi wa Jamii wa Baraza la Wawakilishi Kuhusiana na Utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu wa Mabadiliko ya Kiuchumi (HEET) uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Chuo cha Maruhubi Unguja
Aidha katika kutekeleza Mradi huo Mhe. Mgeni amehimiza kuwepo kwa Mashirikiano ya karibu kati ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA). Pamoja na Wadau mbali mbali wa Elimu ili kuhakikisha utekelezaji wa Mradi huo unakuwa na Matokeo mazuri kwa Lengo la Kuimarisha Maendeleo ya Elimu kwa Ujumla.