Utoaji wa Elimu kwa wanafunzi utapelekea kuengezeka kwa ufaulu mzuri unaoendana samabmba na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.

Amesema hayo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bw. Khamis Abdulla Said. wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Elimu ya Watu Wazima na Siku ya kujua kusoma na kuandika duniani. Iliyo fanyika katika Uwanja wa  Maktaba ya Dunga Wilaya ya kati Unguja.

Amesema, Elimu Bora ni chanzo kikubwa cha mabadiliko katika sekta ya Elimu, hivyo Walimu wajitahidi kusomesha kwa bidii ili kuleta mabadiliko katika sekta hiyo.

Aidha, ametowa wito kwa wazazi na walezi kuwasimamia watoto Katika suala zima la kusoma, kuandika na kuhesabu  ili waweze kuwa imara na kuleta mabadiliko katika masomo yao.

Amesema,  Wizara inafanya jitihada ya kuanzisha Maktaba kwa kila Wilaya ili kuweza kuondoa changamoto ya kufata Maktaba  masafa marefu na kupelekea kuzorotesha maendeleo ya kielimu nchini.

Hata hivyo Katibu Mkuu amewataka Walimu  kuwaongezea muda wa ziada wanafunzi wanaoingia skuli mkondo Mmoja  ili wanafunzi waweze kusoma kwa wakati na kupasi vizuri masomo yao.


Kwa upande wake Mkurugenzi Maktaba Bi. Ulfat Abdul-Azizi Ibrahim amesema, Lengo la Uzinduzi huo ni kuongeza uhamasishaji wa kupenda kusoma na Kuandika ili kuweza kumkomboa Mwanafunzi pamoja na Mwanajamii  ili kuweza kujenga uelewa  na kujikomboa kwa mambo mbali mbali yanayo izunguka jamii kwa ujumla.


Nae Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Mbadala na Watu Wazima Bi. Mashavu Ahmda Fakihi amesema,  uzinduzi huo unatokana na kutaka kutathimni hali ya kisomo katika nchi. pamoja na kuieleza jamii umuhimu wa Elimu ya Watu Wazima ili kuweza kuleta mabadiliko yatayoenda sambamba na ulimwengu wa sasa.


Uzinduzi huo wa madhmisho ya Wiki ya Elimu ya Watu Wazima pamoja na siku ya kujua kusoma na kuandika umefanyika kwa mashirikiano ya Bodi za hudma za Maktba na Idara ya Elimu Mbadala na Watu Wazima.


Ujumbe wa Mwaka huu ni "kukuza uwezo wa kusoma na kuandika kwa mabadiliko ya ulimwengu ili kujenga Msingi ya Jamii Endelevu na yenye amani"


Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano (WEMA).