Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Zanzibar bwana Khamis Abdulla Said amesema, ni muda sasa kwa kila mwalimu kuchukua hatua ili kuhakikisha Zanzibar inaendelea kupata matokeo mazuri zaidi.

Amesema hayo wakati wa kufunga kikao cha tathmini ya nusu mwaka ya Mradi wa kuimarisha ubora wa Elimu ya Sekondari Zanzibar, Katika ukumbi wa mikutano Golden Tulip uwanja wa ndege Mjini Unguja.

Amesema, ili Walimu waendelee kufanya kazi kwa juhudi kubwa Wizara itaendelea kufanya kila namna kwa kushirikiana na wadau mbalimbali  kuhakikisha Walimu nao wanaendelea  kupewa Mafunzo ili kuendana na  mabadiliko ya Teknolojia. 

Amesema, Zanzibar ili iendelee kupata matokeo mazuri ipo haja ya kila muhisika  kutimiza wajibu wake kwa kuengeza bidii zaidi.

Nao washiriki wa kikao hicho wamesema, Serikali inaendelea na jitihada kwa kuimarisha sekta ya Elimu kuanzia miundombinu hadi vifaa vya kujifunzia na kufundishia.

Hivyo ni vyema kwa kuzithamini bidii hizo ili taifa iendelee kupata matokeo mazuri zaidi.

Mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha viongozi mbalimbali wa Wizara ya Elimu Zanzibar, Wawakilishi kutoka KOICA,  Wawakilishi kutoka good Neighbours na wadau mbalimbali wa Elimu nchini.