Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Dkt Mwanakhamis Adam Ameir amesema,  vyombo vya habari vinanafasi kubwa ya  kushajihisha jamii juu ya matumuzi salama ya vidonge vya  virutubisho.


Amesema hayo wakati alipofungua warsha kwa waandishi wa habari juu ya matumuzi salama ya vidonge lishe kwa Wanafunzi Waliobaleghe   huko Kituo Cha Walimu Kiembe Samaki Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.


Amesema, Waandishi wanayo nafasi kubwa kwenye jamii hivyo nao ni njia moja wapo ya kuhakikisha wanafikisha ujumbe husika katika jamii.

 

Aidha amesema, kuipa jamii Taaluma hiyo ni kuepusha dhana potofu iliopo kwenye jamii juu ya matumuzi ya virutubisho hivyo.


Nae Mkuu wa kitengo cha Lishe kutoka Wizara ya Afya Zanzibar bi Asha  Hassan Salmin. akiwajengea uelewa Wandishi hao ametoa  ripoti ya utafiti mdogo juu ya tatizo la ukosefu wa damu kwa Wanafunzi wa kike waliobaleghe amesema, ipo haja ya Wasichana kutumia Virutubishi vya Madini Chuma  mara Bada ya kubaleghe ili kupunguza tatizo hilo nchini.

Warsha hiyo ya siku moja imewashirikisha Waandishi kutoka vyombo  mbalimbali zikiwemo Redio jamii kutoka sehemu mbalimbali.


Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano (WEMA).
Tarehe:03/09/2023