• EMIS
  • E-OFFICE
  • Home
  • About Us
  • News and Events
  • Staff Mail
  • Contact Us
  1. You are here:  
  2. Home
  3. News and Events

MOEVT NEWS&EVENTS

ZIARA YA KATIBU MKUU KATIKA SKULI ZINAZOENDESHA HUDUMA ZA DAKHALIA

Details
01 September 2023
57

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar bwana Khamis Abdulla Said  Leo Tarehe 3108/2023 amefanya ziara katika Skuli zinazoendesha huduma za dakhalia kwa Mkoa wa Mjini Magharib.


Lengo la ziara hiyo ni kuangalia mazingira wanayoishi Wanafunzi hao ambao wanajiandaaa na mitihani yao ya Taifa.


Sambamba na hayo Bwana said alipat fursa ya kwenda kuona mazingira ya Skuli ya Sekondari Dkt salmin amaour ya chumbuni kutokana na kadhia iliojitokeza ya mwanafunzi uumia Bada ya kupandisha mashetana  na kujitupa.

UFUNGUZI WA STUDIO YA 3D

Details
01 September 2023
47

Mkuu wa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia (KIST), Dkt. Mahmoud Abdulwahab Alawi, amesema upo umuhimu mkubwa wa kuwepo studio ya 3D katika Taasisi ya Karume ili kuwawezesha wanafunzi kuongeza ujuzi uliobora katika kukamilisha masomo yao. 

Amesema hayo katika hafla ya ufunguzi wa Studio ya 3D, (iliyofadhidiliwa na Tasisi ya TIKA kutoka nchini Uturky), iliofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa  Dkt Idrissa Muslim Hijja, Mbweni Zanzibar. 

Ameeleza kuwa, kutokana na ukuaji wa teknolojia duniani, Taasisi ya Karume imeona upo umuhimu mkubwa wa kuwafundisha wanafunzi teknolojia ya 3D ili wapate ujuzi wa kisasa utakaowawezesha kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia. 

Aidha, Dk. Mahmoud ametumia fursa hiyo kuipongeza Taasisi ya TIKA kutoka nchini Uturuki kwa kuonesha ushirikiano mzuri kwa Taasisi ya Karume hasa katika miradi ya Elimu.

Read more …

KIKAO CHA TATHMINI YA NUSU MWAKA YA MRADI WA KUIMARISHA UBORA WA ELIMU YA SEKONDARI ZANZIBAR

Details
01 September 2023
51

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dk. Mwanakhamis Adam Ameir amewataka Wadau wa Elimu kuiga mfano wa KOICA wa Kusaidia na  kuimarisha Maendeleo ya Sekta ya  Elimu Zanzibar ili kuengeza Ufaulu kwa Wanafunzi.

Ameyasema hayo wakati alipofungua kikao cha Tathmini ya nusu Mwaka ya Mradi wa Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari Zanzibar iliyofanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip ya Uwanja wa Ndege Mjini Zanzibar.

Amesema KOICA kwa Kushirikiana na Good Neighbers imesaidia sana katika Kuimarisha Maendeleo ya Skuli ikiwemo Kujenga Maabara za Kisasa, Kutoa Mafunzo ya Walimu ya Kuengeza Uwezo wa Kufundishia pamoja na Vifaa na Kuhamasisha Kamati 90 za Skuli za Zanzibar.

Read more …

UZINDUZI WA MIRADI MBALI MBALI KATIKA SEKTA YA ELIMU, " KIZIMKAZI DAY "

Details
30 August 2023
55

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa, leo Tarehe 29/08 /2023, ameshiriki katika Uzinduzi wa Miradi Mbali mbali katika Sekta ya Elimu iliyo zinduliwa na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan.ikiwa ni Shamra shamra za Kizimkazi Day huko Mkoa wa Kusini Unguja.

Miongoni mwa Miradi iliyozinduliwa ni pamoja na  Ujenzi wa Madarasa Sita katika Skuli ya Msingi Muyuni, Ukumbi wa  Mitihani na Chumba cha Kompyuta  katika Skuli ya  Sekondari Muyuni, Maabara ya Tehama, Elimu Mtandao iliyopo Skuli ya Kizimkazi. 


Miradi hiyo Imefadhiliwa na Wadau mbali mbali wa Maendeleo ya Elimu nchini. wakiwemo PBZ Bank, NMB,  TASAF, na (NGO) ya Mwanamke Intiatives Foundation.


Lengo la kujengwa kwa Miradi hiyo ni Kuinyanyua Sekta ya Elimu nchini ili kwenda sambamba na Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia 

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano (WEMA).

ZIARA

Details
29 August 2023
70

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa, leo Tarehe 27/08 /2023 amefanya ziara katika  miradi mbalimbali ya Elimu inayotegea kuzinduliwa na Mhe.dkt Samia Suluhu Hassan.

Miradi hiyo ikiwemo Skuli ya Msingi Muyuni, Holi na Mitihani la Skuli ya  Sekondari Muyini, Maabara ya Tehama, Elimu Mtandao iliyo Kizimkazi iliyofadhiliwa na Mwanamke Foundation. Miradi hiyo itazinduliwa ikiwa ni shamra shamra za Kizimkazi day Mkoa wa Kusini Unguja.

 

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano (WEMA).

Page 5 of 12

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10

Contact Details

P.O.Box 394 Mazizini, Zanzibar
+255 24 223 2827
info@moez.go.tz

Main Menu

  • Home
  • About Us
  • News and Events
  • Staff Mail
  • Contact Us

Get in Touch

P.O.Box 394 Mazizini, Zanzibar
info@moez.go.tz

Our Institute

  • Kwarara Media Education Centre (KMEC)
  • The State University of Zanzibar (SUZA)
  • Vocational Training Authority(VTA)
  • Zanzibar Higher Education Loan Board(ZHELB)
  • Karume Institute of Science and Technology(KIST)
  • Zanzibar Examination Council(ZEC)
  • Zanzibar Institute of Education(ZIE)

External Links

  • Ministry of Education, Science and Technology (MOE)
  • The National Examination Council of Tanzania (NECTA)
  • The National Council for Technical Education (NACTE)
  • Tanzania Commission for University (TCU)
© MoEVT. Designed by ICT-Department.