RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, amesema serikali inatarajia kujenga Skuli 20 zitakazo tumia teknelojia ya vyuma na kuta za dry wall na Gypsam “steal structure”.

Aliyasema hayo katika hafala ya ufunguzi wa Skuli ya Msingi Fuoni Rock, katika shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi, huko Fuoni Mkoa wa mjini Magharibi Unguja.

 

Alisema katika bajeti ya Elimu ya mwaka wa fedha 2024/2025, serikali itaingia mkataba na kampuni ya Rock Development kwa ajili ya ujenzi wa skuli  20 na teknelojia itakayotumika katika ujenzi huo ni tofauti na Skuli zote zinazojengwa.

 

Aidha Dk. Mwinyi alisema ujenzi huo unatumia muda mdogo kukamilika kwake tofauti na ujenzi wa matofali uliozoeleka, pia nchi mbalimbali zimeanza kutumia teknolojia hiyo kwa miaka mingi sasa. 

 

Dk. Mwinyi alisema hatua hiyo itakwenda sambamba na kuziunganisha skuli zote na mkonga wa taifa ili kuimarisha matumizi ya teknolojia katika kufundishia na kujifunzia. 

 

Alifahamisha kuwa, ujenzi wa aina hiyo utasaidia sana nchi katika uhifadhi wa mazingira na kuepuka kutumia mchanga kwa wingi ambao unaathari kubwa ya kimazingira katika visiwa vyetu. 

 

Katika hatua nyingine Dk. Mwinyi amesema, Serikali itaendelea kuajiri walimu1,500  wa fani mbali mbali hasa sayansi katika mwaka huu wa fedha ili kukabiliana na ongezeko la miundombinu ya skuli pamoja na changamoto ya uhaba wa walimu kwa baadhi ya masomo.

Можна взяти мікрокредит на карту будь-якого українського банку та кредит онлайн без відмови, дзвінків та перевірок. На все потрібно 5 хвилин часу.

 

Alibainisha kuwa, Bajeti ya sekta ya elimu imeongezeka kwa asilimia 72.2  kutoka Shilingi 265.5 bilioni mwaka 2021/2022 hadi kufikia Shilingibilioni 457.2 mwaka 2023. 

 

Rais Mwinyi, aliipongeza kampuni ya Rock Development kwa ujenzi wa skuli hiyo, wa majaribio ambao umefanya vizuri na kuzingatia viwango Bora na vya kisasa  vinavyoendana na teknelojia.

 

 

Hata hivyo aliupongeza uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwa kazi nzuri wanayoifanya ikiwemo kuengeza viwango vya ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha sita ambao wamefanya vizuri kwa asilimia 99.

Якщо вам потрібні термінові гроші, наприклад, 10 000 гривень, візьміть кредит на карту, миттєві гроші по всій Україні, щодня без вихідних.

 

Sambamba na hayo aliwataka wananchi kuunga mkono serikali kwani inafanya juhudi kubwa kuhakikisha inaimarisha huduma za elimu nchini kote na kukuyaenzi Mapinduzi ambayo ndio msingi wa Maendeleo kwa wananchi na Serikali.

 

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Muhamed Mussa alisema, aliwapongeza ROCK Development kwa kushirikiana na serikali kujenga jengo la mfano ambalo limetumia teknelojia ya kisasa linalokadiriwa kuwa na umadhubuti wa maiaka 100 ijao.

 

Akitoa salamu za Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,  Mkuu wa Mkoa huo Idrissa Kitwana Mustaffa alisema, jengo la skuli ya Fuoni Rock ndio la kwanza kwa bara la Afrika, Skuli kama hizo zimeonekana nje ya bara la Afrika mfano China.

Взяти онлайн кредит на карту до 50 000 грн. Найкращі пропозиції в Україні. Вигідні кредити готівкою на карту до 35 тисяч під 2% в день.

 

Mwenyekiti wa Rock Development, Enas Ozcan, alisema kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali kujenga miradi mengine mikubwa, kutokana na fursa walioipata hivyo zanzibar itegemee kupata miradi mengine kutoka kwa ROCK.

 

Awali Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, alisema Skuli hiyo ya ghorofa 2 ina urefu wa mita za mraba, 4822 ikiwa na vyumba 29 kila chumba kina uwezo wa kubeba wastani wa wanafunzi 48, Maabara, vyoo, library, Maktaba, Chumba cha kumputa ambapo ujenzi wake umegharimu shilingi Bilioni7.8.