Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar , imeridhishwa na hatua nzuri ya ujenzi wa skuli za Sekondari za ghorofa ( G+3 ) zinazojengwa na Kampuni ya Simba Developers Ltd katika kijiji cha Bumbwini Makoba na Bumbwini Misufini Wilaya ya Kaskazini “ B” Unguja.