• EMIS
  • E-OFFICE
  • Home
  • About Us
  • News and Events
  • Staff Mail
  • Contact Us
  1. You are here:  
  2. Home
  3. News and Events

MOEVT NEWS&EVENTS

Maonesho ni Njia Moja wapo ya Kurahisha na Kusaidia Wanafunzi Kuweza Kupata Huduma za Kitaaluma.

Details
04 August 2023
100

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uchumi na Uwekezaji Mhe Mudrik Ramadhani Soraga amesema maonesho ni njia moja wapo ya  kurahisha na  kusaidia  Wanafunzi kuweza kupata huduma za kitaaluma ili waweze kukamisha ndoto za safar zao za Elimu .


Hayo ameyasema wakati akifanya ziara katika mabanda mbalimbali huko Maisara Mjini Unguja wakati wa maonesho ya 4 ya wiki ya Elimu ya juu Zanzibar.


Amesema maonesho hayo ni Chachu ya kutengeza daraja la juhudi za Serikali ya awamu ya nane Katika sekta ya Elimu nchini.

Ikiwa ni siku ya tatu ya maonesho ya 4 ya wiki ya Elimu ya Juu  vyuo,ambapo  Taasisi mbalimbali za kitaaluma na wajasiriamali  wameshiriki maonesho hayo huko Maisara Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.

Maonesho ya 4  yataleta Mafanikio Makubwa kwa Wanafunzi Kujua Fani zenye Soko la Ajira Duniani.

Details
02 August 2023
80

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe.Simai  Mohamed Said amesema maonesho ya 4  yataleta mafanikio makubwa kwa Wanafunzi wengi kujua namna ya kujiunga na fani zenye soko la ajira duniani.

Amesema hayo wakati alipotembelea mabanda mbalimbali ya maonesho ya Nne ya wiki ya Elimu Zanzibar huko Maisara Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.

Amesema uwepo wa taaluma ambayo itasaidia Wanafunzi kujua vipaombele vya Serikali ili taifa lizalishe wataalam wazalendo.

Read more …

Uhaba wa Wataalamu wa wa Sayansi nchini hupelekea kuzorotesha kasi ya Maendeleo.

Details
02 August 2023
92

Uhaba wa Wataalamu wa wa Sayansi nchini hupelekea kuzorotesha kasi ya Maendeleo.

Amesema hayo Daktari bingwa wa Meno Zanzibar. Dr  Semeni Shaabani Mohammed ambae ni Mtu wa Mfano alliyefanikiwa katika Masomo ya Sayansi (Role Model). wakati wa muendelezo wa  Ziara ya kuwahamasisha Wazazi katika kuwaandaa Watoto wa Kike kuyapenda na kuyasoma Zaidi Masomo ya Sayansi.


Ziara  hiyo imefanyika katika Skuli ya Mtoni Kigomeni, Mwenge, Mfenesi, Bubwini Makoba, Donge na Muwanda kwa Upande wa Unguja.

Amesema, Dunia  Sasa inaendana na Kasi ya Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia hivyo Wanafunzi lazima wasome kwa bidii ili kupata wataalamu watakaoisaidia nchi kuendana na kasi ya maendeleo.

Read more …

Ziara ya Kutembelea miradi ya ujenzi inayoendelea katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Details
02 August 2023
102

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Ali Abdulgulam Hussein amesema  atahakikisha anafuatilia miradi yote iliyopo chini ya Wizara ya Elimu ili ipatikane kwa wakati.

Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi inayoendelea katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Amesema  ili miradi  ipatikane kwa wakati ni lazima kuwepo kwa mashirikiano baina ya Wizara na Wakandarasi waliopewa miradi hiyo sambamba na ufuatiliaji wa  mara kwa mara ili kuweza kuskiliza na kuzipatia ufumbuzi wa haraka changamoto mbalimbali zinazijitokeza katika miradi hiyo.

Read more …

Hafla ya Ugawaji wa Vifaa vya Maabara kwa Skuli ya Sekondari Jongowe, Tumbatu

Details
02 August 2023
98

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Ali Abdulgulam Hussein   amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuhakikisha sekta ya Elimu inaendelea kupiga hàtua.

Amesema hayo wakati wa hafla ya Ugawaji wa vifaa vya maabara kwa Skuli ya Sekondari Jongowe Wilaya ndogo Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Amesema  Serikali ya awamu ya nane imekusudia kuboresha miundombinu  ya Skuli na upatikanaji wa vifaa vya kufundishia ili taifa lizalishe wataalam wazalendo.

Aidha amesema upatikanaji wa vifaa vya kufundishia vitaleta ufanisi katika kukuza kiwango cha ufaulu nchini.

Read more …

Page 8 of 12

  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12

Contact Details

P.O.Box 394 Mazizini, Zanzibar
+255 24 223 2827
info@moez.go.tz

Main Menu

  • Home
  • About Us
  • News and Events
  • Staff Mail
  • Contact Us

Get in Touch

P.O.Box 394 Mazizini, Zanzibar
info@moez.go.tz

Our Institute

  • Kwarara Media Education Centre (KMEC)
  • The State University of Zanzibar (SUZA)
  • Vocational Training Authority(VTA)
  • Zanzibar Higher Education Loan Board(ZHELB)
  • Karume Institute of Science and Technology(KIST)
  • Zanzibar Examination Council(ZEC)
  • Zanzibar Institute of Education(ZIE)

External Links

  • Ministry of Education, Science and Technology (MOE)
  • The National Examination Council of Tanzania (NECTA)
  • The National Council for Technical Education (NACTE)
  • Tanzania Commission for University (TCU)
© MoEVT. Designed by ICT-Department.