
- Details
- 69
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh. Lela Mohammed Mussa amepiga marufuku Vyuo vya hapa nchini kuondoa masomo ya dini na kiarabu katika kutangaza fani zao.
Waziri Lela ameyasema hayo katika uzinduzi wa Maonesho ya Elimu ya Juu uliofanyika katika kiwanja Cha Gombani Chake Chake Pemba.
Amesema imekuaa ni kawaida kwa baadhi ya Vyuo kutangaza fani zao huku wakiainisha Masomo ya Dini na Kiarabu kua hayahitajiki hivyo amevitaka Vyuo hivyo kuacha Mara moja tabia hiyo.
Akifafanua zaidi Waziri Lela amesema tabia hiyo imekua ikiwakatisha tamaa Wanafunzi wa Skuli za Msingi na Sekondari na kuacha kuyasoma Masomo hayo wakiamini kwamba hayahitajiki katika maisha yao.
Amesema Licha ya ukweli kwamba fani zao hazihitaji Masomo hayo hawatakiwi kutangaza kwamba Masomo hayo hayahitajiki.