- Detalles
- 385
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Abdulgulam Hussein amesema ni haki ya Msingi kila binaadam kupata hifadhi ya jamii.
Amesema hayo wakati wa hafla ya ufunguzi wa klabu za pencheni za ZSSF ikiwa ni shamrashamra za kutimiza miaka 25 tokea kuanzishwa mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar (ZSSF) . katika ukumbi wa kariakoo Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.
Amesema, Mfuko wa hifadhi pia una haki ya kutoa taaluma kwa jamii kwani mfuko wa hifadhi ni haki ya kila mtu kwa mujibu wa mipango ya nchi husika.
Aidha amewasisitiza Wanafunzi kuwa mabalozi wazuri wa kuelimisha jamii juu ya kijiunga na mfuko wa hifadhi.