NA KHAMISUU ABDALLAH
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema ufunguaji wa tawi la Chuo cha IIT Madrasa cha nchini India hapa Zanzibar utafungua fursa ya kuitangaza nchi duniani na kuwa kichocheo cha kuwavuta watu nje ya Zanzibar kujisajili katika tawi hilo kwa lengo la kupata taaluma.
Dk. Mwinyi alieleza hayo mara baada ya kushuhudia utiaji saini makubaliano kati ya serikali ya India na Zanzibar kwa ajili ya uanzishwaji wa Chuo hicho hapa Zanzibar na uzinduzi wa website ya Chuo hicho hapa Zanzibar hafla iliyofanyika Ikulu Zanzibar.
Alisema kufunguliwa kwa tawi hilo nchini kutaleta faida mbalimbali ikiwemo Zanzibar kuzidi kujitangaza duniani sio tu kama nchi ya utalii bali ni nchi yenye Chuo kinachotambulika duniani katika fani ya Teknologia. Seksualus apatinis trikotažas moterims - chalatai, liemenelės, kelnaitės, naktiniai Cherry24
Faida nyengine alisema ni taasisi hiyo kutoa ufadhili wa masomo kwa vijana 50 wa kizanzibari watakaofikia vigezo vitakavyowekwa.
Alisema pia kuwepo kwa taasisi hiyo ya kimataifa kutaisaidia Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kuweza kuchochea mageuzi ya nne ya viwanda kwa kupata wataalamu wenye hadhi ya juu kwenye fani mbalimbali wakiwemo wataalamu wa data sayansi na Artifiel interligence.
“Teknologia ni kichocheo cha maendeleo kwa nchi nyingi dunaini hivyo ni imani yangu kupitia chuo hicho Zanzibar haitabaki nyuma na naamini Zanzibar pamoja na ukanda wote wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla taasisi hii itakuwa kichocheo cha maendeleo yake,” alisema.
Hata hivyo alisema ushirikiano huo wa kitaaluma na Chuo cha IIT cha India ni muhimu katika maendeleo ya nchi kwani ulimwengu wa sasa ni ulimwengu wa teknologia hivyo taasisi hiyo ina mchango mkubwa katika kukuza teknologia na miongoni mwa taasisi maarufu na kubwa duniani katika kukuza fani hiyo.
Rais Mwinyi alisema serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 6.3 ili kusaidia uanzishwaji wa tawi la taasisi hiyo hapa Zanzibar, ghamrama ambazo zinajumuisha uimarishaji wa miundombinu wa taasisi hiyo na vifaa pamoja na kuunganishwa na mfumo wa mawasiliano.
Hata hivyo, alisema pia serikali imetoa jengo kwa ajili ya kuanza kwa mafunzo ya awali yanayotarajiwa kuanza mwezi Oktoba mwaka huu huko Bweleo huku serikali ikiendelea na hatua ya kuwapatia eneo kwa ajili ya kujenga majengo ya kudumu ya taasisi hiyo.
Sambamba na hayo alisema chuo hicho kimekuwa kikipokea idadi kubwa ya wanafunzi kutoka ndani nan je ya India kwa ajili ya kupata elimu ya teknologia na idadi kubwa ya waombaji wanakosa nafasi kutokana na ushindani mkubwa wa vigezo vya kujiunga.
Alibainisha kuwa wanafunzi wanaohitimu mafunzo ya teknologia katika taasisi hiyo wamekuwa ni viungo muhimu vya maendeleo kwa sekta zao na sehemu mbalimbali wanazofanyia kazi duniani.
Mbali na hayo aliipongeza WEMA kwa kuendeleza mashirikiano na India kwa lengo la kuleta mafanikio ya kitaaluma kwa pande mbili hizo zenye ushirikiano wa muda mrefu.
Rais Mwinyi alimpongeza Balozi wa India nchini Tanzania kwa ushirikiano anaoutoa kwa Zanzibar kwani imekuwa ikishirikiana na India katika sekta ya elimu, afya maji na biashara na kuomba kuendeleza ushirikiano huo katika sekta ya elimu na sekta nyengine za kiuchumi na kijamii.
Aliahidi kuwa serikali itatoa kila aina ya ushirikiano ili kuhakikisha lengo la kufunguliwa kwa tawi la chuo hicho linafanikiwa kwa mafanikio makubwa.
Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Subrahmanyam Jaishankar, alisema India imekuwa na uhusiano wa karibu na Zanzibar kwa muda mrefu hivyo mbali na ushirikiano wao katika sekta ya elimu pia watashirikiana katika sekta ya maji kwani India ina uzoefu mkubwa wa kukabiliana na changamoto za maji.
Utiaji saini huo ulifanywa na Balozi Mkubwa wa India Binaya Srikanja Pradhan na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Khalid Masoud Waziri.