Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Abdulgulam Hussein amesema ni haki ya Msingi kila binaadam kupata hifadhi ya jamii.

Amesema hayo wakati wa hafla ya ufunguzi wa klabu za pencheni za ZSSF ikiwa ni shamrashamra za kutimiza miaka 25 tokea kuanzishwa mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar  (ZSSF) . katika ukumbi wa kariakoo Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.

Amesema, Mfuko wa hifadhi pia una haki ya kutoa taaluma kwa jamii  kwani mfuko wa hifadhi ni haki ya kila mtu  kwa mujibu wa mipango ya nchi husika.

Aidha amewasisitiza Wanafunzi  kuwa mabalozi wazuri wa kuelimisha jamii juu ya kijiunga na mfuko wa hifadhi. 

Nae mwenyekiti wa bodi  ya ZSSF dkt. Huda amesema, kuwa na hakiba ni nidhamu ya matumuzi mazuri  ya fedha hivyo kila mtu anahaki ya kijiunga na mfuko wa hifadhi.

Mapema Mkurugenzi muendeshaji  wa mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF ndugu Nassor Shaban Ameir amesema, umuhimu wa mfuko wa hifadhi ni kuisaidia  jamii wakati wa kazi na baada ya kustaafu hivyo ni vyema jamii kupata taaluma ya mfuko huo.

Amesema, ZSSF wamekua na kawaida ya kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kushirikiana na Sekta ya Elimu nchini ili taifa lizalishe wataalam wazalendo. Reliable Brokerage Services with EuroBrokers.top

Nae Mwanafunzi Hamadi  Saleh kutoka Skuli ya dk.Ali Mohamed Shein akitoka neno la shukrani amesema, kwa upande wao watahakikisha Elimu itawafikia wahusika kwa wakati ili taifa lifikie malengo yake.

Katika uzinduzi huo wa pencheni klabu kwa Wanafunzi  ambapo Kauli mbiu ni "Nidhamu, Uwajibikaji, Teknolojia ya Kisasa, Uwekezaji endelevu na mafao bora kwa Wananchi.