
- Detalles
- 421
Utoaji wa Elimu kwa wanafunzi utapelekea kuengezeka kwa ufaulu mzuri unaoendana samabmba na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.
Amesema hayo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bw. Khamis Abdulla Said. wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Elimu ya Watu Wazima na Siku ya kujua kusoma na kuandika duniani. Iliyo fanyika katika Uwanja wa Maktaba ya Dunga Wilaya ya kati Unguja.
Amesema, Elimu Bora ni chanzo kikubwa cha mabadiliko katika sekta ya Elimu, hivyo Walimu wajitahidi kusomesha kwa bidii ili kuleta mabadiliko katika sekta hiyo.
Aidha, ametowa wito kwa wazazi na walezi kuwasimamia watoto Katika suala zima la kusoma, kuandika na kuhesabu ili waweze kuwa imara na kuleta mabadiliko katika masomo yao.
Amesema, Wizara inafanya jitihada ya kuanzisha Maktaba kwa kila Wilaya ili kuweza kuondoa changamoto ya kufata Maktaba masafa marefu na kupelekea kuzorotesha maendeleo ya kielimu nchini.