
- Detalles
- 363
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa amesema, Kuoengezeka kwa kiwango cha ufaulu Zanzibar kutapelekea Kupiga hatua nzuri ya Kimaendeleo nchini.
Ameyasema hayo wakati wa hafla ya kuwapongeza Walimu wa Kidato cha Sita kwa upande wa Unguja kwa Matokeo mazuri ya mwaka 2022/2023. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari Lumumba Mjini Unguja.
Amesema, ufaulu wa Kidato cha Sita umeongozeka kwa kiasi kikubwa jambo ambalo litapelekea kupatikana kwa Wataalamu bora nchini.
Aidha amesema, Walimu bado wanakazi kubwa ya kuleta Mageuzi katika Sekta ya Elimu yenye kumlenga Mtoto katika kupata Elimu Bora itakayomsaidia katika maisha yake ya baadae.
Amesema, Wizara inatambua uwepo changamoto ya Maabara kwa wanafunzi wa Sayansi. Hata hivyo Serikali inajitahidi kujenga Maabara za kisasa kuanzia ngazi ya Msingi hadi Sekondari ili kuleta ufaulu mzuri wa wanafunzi katika masomo hayo.