
- Detalles
- 688
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Muhamed Mussa amesema michezo ni njia moja yakuleta maendeleo nchini.
Amesema hayo wakati wa kufunga Michuano ya ZAHILFE Cup kwa Upande wa Chuo cha Mwalimu Nyerere na chuo cha Zanzibar (ZU) yaliyo fanyika Katika Uwanja wa Mao Zedong Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.
Amesema , Vijana wanapokusanyika pamoja kwa lengo la kushirikiana ili kuhakikisha wanaendeleza gurudumu la maendeleo kwa taifa lao.
Amesema, Michezo huleta umoja , amani na mashirikiano hivyo ni vyema kufata kanuni za michezo ili kuhakikisha michuano hiyo inaendelea kuleta maendeleo nchini.