Muhasibu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar bwana Said Seif Said amefanya ziara na kuzungumza na wahasibu wake wote wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na wa katiba nasheria Katika ukumbi wa Wizara ya Elimu Mazizini Unguja.
Lengo la ziara hiyo ni kuweza kujua tathmini ya mwaka wa fedha 2022-2023, kujua changamoto mbalimbali za kazi.
Aidha amewasisitiza kufanya Kazi kwa bidii katika mwaka mpya wa fedha 2023-2024 na kufata na sheria na taratibu ili kuweza kuondoa mapungufu yalojitokeza.