Title Image
Untitled Document

TANGAZO

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar inawatangazia wanafunzi wote wanaohitaji kujiendeleza katika fani mbalimbali za Elimu ya Juu kuwa fomu za maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/18 zitaanza kutolewa kwa miezi mitatu kuanzia tarehe 02/05/2017 hadi tarehe 31/07/2017.

Mikopo itatolewa kwa waombaji waliotimiza sifa za kujiunga na masomo ya juu katika ngazi za:

 • Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree),
 • Shahada ya Pili (Master Degree)
 • Shahada ya Tatu (PhD).

Walengwa wa maombi ya mikopo ni:

 • Wahitimu wa Kidato cha Sita wenye sifa za kujiunga na masomo ya Shahada ya Kwanza.
 • Wahitimu wa Diploma wenye sifa za kujiunga na masomo ya Shahada ya Kwanza.
 • Wahitimu wa Shahada ya Kwanza wenye sifa za kujiunga na masomo ya Shahada ya Pili.
 • Wahitimu wa Shahada ya Pili wenye sifa za kujiunga na Shahada ya Tatu.

Kuanzia mwaka wa masomo 2017/18 Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar haitatoa mikopo kwa waombaji ambao ni watumishi wa Taasisi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT). Mkazo umewekwa kwa vijana wapya waliomaliza masomo na ambao hawajapata ajira.

Waombaji wa mikopo wanapaswa kuzingatia Fani za Vipaumbele vya Serikali ambazo zinapatikana katika tovuti za Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar (www.zhelb.go.tz) na tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar (www.moez.go.tz).

Fomu za maombi zitalipiwa shilingi 10,000 ambazo zitalipwa moja kwa moja na muombaji kwenye akaunti namba 021108001357 ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu iliyopo katika Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

Wanaohitaji fomu za maombi wanaombwa kufika katika ofisi za Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu zilizopo Vuga kwa Unguja na jengo la Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Chakechake Pemba na wanatakiwa kuchukua:

 • Kitambulisho cha Mzanzibari
 • Fomu ya malipo (Pay Slip) kutoka Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ)
 • Vivuli vya vyeti na matokeo ya masomo kwa ngazi aliyohitimu.

SIFA ZA KUPATA MKOPO

Sifa za waombaji wa mikopo ambao maombi yao yanaweza kuzingatiwa wakati wa uteuzi zimetajwa kwenye kifungu cha 20 zikiwemo:

 • Mwombaji awe Mzanzibari
 • Awe ameomba mkopo kwa kujaza Fomu Namba 1 au kupitia njia nyengine yoyote ile ambayo BMEJZ itaona inafaa. Maombi yawe yamewasilishwa ndani ya muda maalum uliowekwa na BMEJZ unaoanzia Mei 2 hadi Julai 31 ya kila mwaka.
 • Awe amepata udahili kwenye chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa na mamlaka husika nchini.
 • Awe amepata alama nzuri za ufaulu.
 • Mwombaji wa shahada ya kwanza (Bachelor/First Degree) aliyehitimu kidato cha sita anapaswa awe amefaulu angalau masomo mawili (Principal subjects) kwa alama za ufaulu zinazoanzia:
 • alama 4.0 kwa wahitimu wa masomo ya sayansi au ufundi;
 • alama 5.0 kwa wahitimu wa masomo ya biashara;
 • alama 5.0 kwa wahitimu wa masomo ya sanaa au sayansi jamii.
 • Mwombaji wa shahada ya kwanza aliyehitimu stashahada ya kawaida (Ordinary Diploma) katika masomo ya sayansi au ufundi anatakiwa awe na ufaulu wa alama (GPA) 3.0 au B; wahitimu wa stashahada za masomo ya biashara, sayansi jamii au Sanaa wapate alama kuanzia 3.5 au B+.
 • Mwombaji wa shahada ya uzamili (Master/Second Degree) katika masomo ya sanaa au sayansi jamii awe amehitimu shahada ya kwanza na kupata alama za ufaulu kuanzia daraja la pili la juu (upper second class). Waombaji wa shahada ya uzamili katika nasomo ya sayansi, ufundi, tiba, uchumi, mipango na biashara wawe na alama za ufaulu za kuanzia daraja la pili la chini (lower second class). Wahitimu wa stashahada ya uzamili wanapaswa kupata alama za ufaulu kuanzia daraja la pili la chini (lower second class)
 • Mwombaji wa shahada ya uzamivu (Doctor of Philosophy - PhD) awe amehitimu shahada ya uzamili na kupata alama za kuanzia daraja la pili la juu kwa waombaji wa masomo ya sanaa na sayansi jamii. Waombaji wa shahada ya uzamivu katika masomo ya sayansi, ufundi, udaktari na uchumi, mipango na takwimu wapate alama za ufaulu kuanzia daraja la pili la chini.
 • Waombaji wanaoendelea na masomo vyuoni pia wanaweza kuomba kwa kuzingatia sifa za kitaaluma zilizotajwa hapo juu [d(i) –(iv)]. Aidha mwombaji awe amefaulu mitihani yake ya chuo kwa kiwango kitakachomwezesha kuendelea na masomo kwa mwaka unaofuatia katika ngazi ya masomo anayoombea mkopo.
 • Awe ameomba fani inayolingana na vipaumbele vya SMZ katika mwaka husika.
 • Asiwe na mkopo au udhamini wa masomo kutoka taasisi nyengine.
 • Mwombaji wa shahada ya kwanza asizidi umri wa miaka 40 kuanzia tarehe ya kutuma maombi na mwombaji wa shahada ya uzamili asizidi miaka 45 kuanzia tarehe ya kutuma maombi. Ukomo wa umri wa mwombaji wa shahada ya uzamivu ni miaka 47 kuanzia tarehe ya kutuma maombi.
 • Mwombaji aliyeajiriwa kwenye utumishi wa umma awasilishe barua ya ruhusa kutoka kwa mwajiri wake.
 • Mwombaji anayedaiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar awe ameshaanza kulipa deni lake kwa angalau asilimia 25 ya deni lote bila ya kusita kwa malipo ya deni ya kila mwezi.
 • Mwombaji aliyesoma kwa mkopo kutoka BMEJZ awe ameshafanya kazi kwa angalau miaka miwili baada ya kuhitimu masomo yake ya awali kabla ya kuomba mkopo mwengine kutoka BMEJZ.

Angalizo:

 • Waombaji wanaotumia sifa za masomo ya kidato cha nne kuomba udahili katika vyuo vikuu vya nje ya nchi ili kujiunga na masomo ya Shahada ya Kwanza, maombi yao ya mkopo hayatozingatiwa.
 • Waombaji wa mikopo waliohitimu masomo ya Diploma pasi na kuwa na elimu ya kidato cha sita au sifa za kujiunga na kidato cha sita, wanatakiwa wawe wamefaulu angalau masomo matano ya Kidato cha Nne kwa kiwango cha alama D na kuhitimu ngazi ya cheti (Certificate) kabla ya kujiunga na masomo ya Diploma.
 • Waajiriwa hawahusiki na utaratibu wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka huu wa masomo

FANI ZA VIPAUMBELE WA KIPINDI CHA 2016 - 2020

Tume ya Mipango ya SMZ imetoa taarifa kuhusu utafiti uliofanywa juu ya hali ya utumishi nchini ambayo imeonesha uwepo wa mahitaji makubwa ya wataalamu. Taarifa hiyo imeibua maeneo ya Vipaumbele vya SMZ juu ya mahitaji ya wataalamu na imeagizwa kuwa taarifa hiyo itumike kama kigezo muhimu kwa utoaji wa mafunzo ya elimu ya juu nchini ili kufikia utekelezaji wa mipango na maendeleo ya rasilimali watu iliyo bora na itakayowaandaa watu wenye ujuzi sahihi, taaluma, tabia na silka zenye tija zinazoendana na mabadiliko ya mfumo wa ushindani wa soko la ajira na kufikia viwango vya juu vya uzalishaji na utoaji huduma.

Ili kurahisisha utekelezaji wa Vipaumbele vya SMZ katika utoaji wa mafunzo ya elimu ya juu kuanzia mwaka wa masomo 2016/17 hadi 2019/20, Tume ya Mipango imevigawa vipaumbele hivyo katika madaraja matatu tofauti kulingana na umuhimu wa kila kada kama inavyoonekana katika jedwali la hapo chini.

Hivyo, kwa mwaka huu wa masomo, BMEJZ itazingatia kikamilifu taarifa ya Tume ya Mipango wakati wa upokeaji wa maombi ya mikopo na uteuzi wa waombaji katika mwaka wa masomo 2017/18. 


SEKTA

FANI NA KIWANGO CHA KIPAUMBELE

DARAJA LA KWANZA

DARAJA LA PILI

DARAJA LA TATU

EDUCATION

Science and Mathematics

Curriculum Development

Learning Material development

 

Technical Vocational Training

School science Laboratory Management

 

 

Early Primary Education

 

 

 

Geography and English language

 

 

HEALTH

Anaesthesiology

Cardiology

Biochemist

 

Dentist

Dermatology

Chemistry

 

Gastroenterology

Endocrinology

ENT

 

Haematology

General Surgeon

General Medicine

 

Medical imaging

Medical Emergency

Infectious diseases

 

Neurosurgery

Oncology

Microbiology

 

Obstetrics and Gynaecology

Paediatric surgery

Nephrology

 

Opthalmology

Physiotherapy

Pharmacology

 

Orthopaedic

Psychiatry

Pharmacy

 

Pathology

Neurology

Plastic surgery

 

Radiology

 

Rheumatology, Allergy and immunology

 

Urology

 

Virology

LAND AND ENERGY

Cartography

Architect

Environment health surveying

 

Land Management

Mining/metallurgy engineering

 

 

Land surveying

Quantity surveying

 

 

Urban Planning

Radiation protection

 

 

 

Renewable Energy and Atomic Energy

 

PETROLEUM AND GAS

Geology

 

 

 

Petroleum chemistry

 

 

 

Petroleum engineering

 

 

 

Geophysics

 

 

 

Petroleum economics

 

 

 

Environmental engineering (Oil and Gas)

 

 

INDUSTRIES

Biological/Chemical Laboratories technicians

 

 

 

Chemical Engineering

 

 

 

Industrial Engineering (Production, Quality Assurance, Product Design)

 

 

 

Soil expertise

 

 

 

Water Engineering

 

 

 

Water management

 

 

TRADE

Trade Economics

International Business

Trade Administration

TOURISM

Tourism Marketing

Language Professions

 

 

Cultural heritage and Conservation

Tourism management

 

 

Hospitality

 

 

 

Tourism Planning

 

 

AGRICULTURE

Aquaculture

Agro forests

Agriculture planning

 

Irrigation Engineering

Animal breading

Agronomy

 

Plant Breeding

Animal Nutrition

Animal Husbandry

 

Plant Pathology

Biotechnology

Fisheries Science

 

Soil science Disciplines

Entomologist

Marine Science

 

 

Food and nutrition

Seed technology

 

 

Horticulture

 

 

 

Microbiologist

 

 

 

Natural resources management

 

 

 

Veterinary

 

Finance

Financial market and investment

Insurance

Banking and Business Administration

 

Financial Management

Procurement

 

 

Programme analysis

Risk and  damage evaluation

 

Transport and Communication

Computer Science and engineering

Port and shipping management

 

 

Information, Communication Technology (ICT)

Road economists

 

 

Telecommunication engineering

Pilot and Aircraft Engineering

 

Environment

Natural resources management

Environment Impact Assessment

 

 

 

Environment Planning and Management

 

 

 

Waste management

 

Economics and Development Planning

Monitoring and Evaluation

Building Economics

 

 

Specialized Economics (Educational health, development etc).

Entrepreneur

 

 

Statistics

Human Resource Management, Planning and Development

 

 

 

International Development Policy and Negotiation

 

 

 

Local Government

 

Other professional

 

 

Mass Communication

 

 

 

International Relation