
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kupitia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuimarisha na kusimamia upatikanaji wa huduma ya elimu bora kwa wananchi wa Zanzibar.
Ameyasema hayo Mkurugenzi Mtendaji Baraza la Mitihani Zanzibar Ndg.Rashid A. Mukki wakati akitangaza rasmi matokeo ya Mtihani wa Taifa ya Darasa la Saba kwa mwaka 2025, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Elimu Mazizini – Unguja.
Wakati akitangaza matokeo hayo Mkurugenzi amesema, Mtihani wa Darasa la Saba kwa mwaka 2025 ulianza tarehe 15/09/202: hadi tarehe 18/10/2025 na jumla ya
Vituo vya mitihani vilivyosajiliwa 514. Skuli za Serikali 299 na Binafs 215. vituo 36 vimeongezeka (7.53%) ukilinganisha na vituo 478 vilivvosaiiliwa mwaka 2024
Amesema, Jumla ya watahiniwa 53,456 walisajiliwa. Wanawake 27,144 (50.78% na wanaume 26,312 (49.22%). Watahiniwa 6,508 (12.17% wameongezeka ikilinganishwa na watahiniwa 46,948, waliosailiwa mwaka 2024. Watahiniwa 46,896 (87.73%) kutoka Skuli za Serikali na 6,560 (12.27%) wa skuli za Binafsi.
Amesema kwa upande wa
Watahiniwa wenye mahitaji maalumu, Wanafunzi waliosajiliwa 296. wakiwema wasioona 05, ulemavu wa viungo 22, ulemavu mchanganyiko 04, viziwi 38, ulemavu wa akili 85 na uoni hafifu 142. Kumekuwa na ongezeko la watahiniwa wenye woni hafifit kwa (94.52%).
Aidha amesema, Watahiniwa 52,374 walifanya mtihani, Wanawake 26,862 (51.29%) na 25,512 (48.71%) wanaume. Watahiniwa wameongezeka 6,353 (13.81%) ikilinganishwa na mwaka 2024. Watahiniwa 45,845 (87.53%) kutoka Skuli za Serikali na 6,529 (12.47%) kutoka skuli Binafsi,
Akizungumzia mahudhurio ya Watahiniwa amesema, Watahiniwa 1,082 (2.02%) hawakuhudhuria kufanya mitihani. Asilimia (73.94%) ya watahiniwa watoro ni wanaume na 26.06% wanawake ambao hawakufanya mtíhani wa mwaka 2025.
Amesema Baraza la Mitihani la Zanzibar katika kikao chake cha 49 limeidhinisha matokeo ya mtihani wa Darasa la Saba ya mwaka 2025 ambapo matokeo yanaonesha kuwa watahiniwa 50,769 (96.94%) wamefaulu. Ufaulu huo umepanda kwa (0.28%) kuliganisha na matokeo ya mtihani ya mwake 2024. Asilimia ya ufaulu ilikuwa 96.66%. Pia, ufaulu wa chin amepunguwa kwa (0.28%) ulinganishwa na ufaulu wa (3.34%) wa mwaka 2024, Ufaulu wa watahiniwa wa jinsia ya kike upo juu kwe (52.36%) ukilinganisha na watahiniwa wa jinsia ya kiume (47.64%)
Amesema Ufaulu wa madaraja ya A, B na F umeimarika kama ifuatavyo:
a) Watahiniwa 314 (0.60%) wamefaulu kwa wastani wa iuu wa Daraia A hili ni ongezeko la (0.1%).
b) Watahiniwa 5,975 (11.41%) wamefaulu kwa wastani wa Daraja B ni ongezcko la (0.95%).
c) Watahiniwa wengine 21,839 (41.70%) wamcfaulu kwa wastani unaoridhisha wa Daraja C
d) Watahiniwa waliobakia 22,641 (43.23%) wamefaulu kwa wastani wa chini wa Daraja D na
c) Watahiniwa 1,605 (3.06%) wamepata wastani wa chini kabiss usioridhisha wa Daraja F,
Amesema Ufaulu wa masomo unaonesha kuwa somo la Sanaa za Ubunifu na Michczo lina ufaulu wa juu zaidi Wa 99.02% Somo la Hisabati lina
ufaulu wa 59.69%, Ufaulu wa somo hilo umepanda kwa 4.17% kulinganisha na ufaulu wa mwaka 2024 wa 55.52%.
Akizungumzia ufaulu wa wanafunzi wenye mahitaji Maalum amesema Ufaulu unaonesha kuwa kati ya watahiniwa 294 wenye mahitaii maalum watahiniwa 280 (95.24%) wakiwemo wasiona 5, ulemavu wa viungo 19. viziwi 36, uoni hafifu 136, ulemavu mchanganyiko 3 na ulemavu wa akili 85.
Kwa ujumla Baraza la Mitihani la Zanzibar linatoa shukrani kwa Uongozi.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano WEMA.