Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bw. Khamis Abdulla Said, amefanya ziara ya Kushtukiza katika Skuli ya Sekondari Mwera, ili kuona changamoto zinazowakabili nakuzitafutia ufumbuzi. Katika ziara hiyo, pia Katibu Mkuu ameonana na Walimu wanofanya mafunzo kwa vitendo na kuwataka kuacha kufanya kazi kwa mazowea. Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano (WEMA).
Серед позичальників популярною послугою став мікрокредит онлайн на картку в мікрофінансовій організації. В банках такого поки що нема. Как в сегодняшних реалиях оформить микрозайм без отказа с мгновенным решением? Посмотрите лучшие предложения на нашем сайте.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar bwana Khamis Abdulla Said Leo Tarehe 3108/2023 amefanya ziara katika Skuli zinazoendesha huduma za dakhalia kwa Mkoa wa Mjini Magharib.
Lengo la ziara hiyo ni kuangalia mazingira wanayoishi Wanafunzi hao ambao wanajiandaaa na mitihani yao ya Taifa.
Sambamba na hayo Bwana said alipat fursa ya kwenda kuona mazingira ya Skuli ya Sekondari Dkt salmin amaour ya chumbuni kutokana na kadhia iliojitokeza ya mwanafunzi uumia Bada ya kupandisha mashetana na kujitupa.
Mkuu wa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia (KIST), Dkt. Mahmoud Abdulwahab Alawi, amesema upo umuhimu mkubwa wa kuwepo studio ya 3D katika Taasisi ya Karume ili kuwawezesha wanafunzi kuongeza ujuzi uliobora katika kukamilisha masomo yao.
Amesema hayo katika hafla ya ufunguzi wa Studio ya 3D, (iliyofadhidiliwa na Tasisi ya TIKA kutoka nchini Uturky), iliofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa Dkt Idrissa Muslim Hijja, Mbweni Zanzibar.
Ameeleza kuwa, kutokana na ukuaji wa teknolojia duniani, Taasisi ya Karume imeona upo umuhimu mkubwa wa kuwafundisha wanafunzi teknolojia ya 3D ili wapate ujuzi wa kisasa utakaowawezesha kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia.
Aidha, Dk. Mahmoud ametumia fursa hiyo kuipongeza Taasisi ya TIKA kutoka nchini Uturuki kwa kuonesha ushirikiano mzuri kwa Taasisi ya Karume hasa katika miradi ya Elimu.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dk. Mwanakhamis Adam Ameir amewataka Wadau wa Elimu kuiga mfano wa KOICA wa Kusaidia na kuimarisha Maendeleo ya Sekta ya Elimu Zanzibar ili kuengeza Ufaulu kwa Wanafunzi.
Ameyasema hayo wakati alipofungua kikao cha Tathmini ya nusu Mwaka ya Mradi wa Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari Zanzibar iliyofanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip ya Uwanja wa Ndege Mjini Zanzibar.
Amesema KOICA kwa Kushirikiana na Good Neighbers imesaidia sana katika Kuimarisha Maendeleo ya Skuli ikiwemo Kujenga Maabara za Kisasa, Kutoa Mafunzo ya Walimu ya Kuengeza Uwezo wa Kufundishia pamoja na Vifaa na Kuhamasisha Kamati 90 za Skuli za Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa, leo Tarehe 29/08 /2023, ameshiriki katika Uzinduzi wa Miradi Mbali mbali katika Sekta ya Elimu iliyo zinduliwa na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan.ikiwa ni Shamra shamra za Kizimkazi Day huko Mkoa wa Kusini Unguja.
Miongoni mwa Miradi iliyozinduliwa ni pamoja na Ujenzi wa Madarasa Sita katika Skuli ya Msingi Muyuni, Ukumbi wa Mitihani na Chumba cha Kompyuta katika Skuli ya Sekondari Muyuni, Maabara ya Tehama, Elimu Mtandao iliyopo Skuli ya Kizimkazi.
Miradi hiyo Imefadhiliwa na Wadau mbali mbali wa Maendeleo ya Elimu nchini. wakiwemo PBZ Bank, NMB, TASAF, na (NGO) ya Mwanamke Intiatives Foundation.
Lengo la kujengwa kwa Miradi hiyo ni Kuinyanyua Sekta ya Elimu nchini ili kwenda sambamba na Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano (WEMA).