• EMIS
  • E-OFFICE
  • Home
  • About Us
  • News and Events
  • Staff Mail
  • Contact Us
  1. You are here:  
  2. Home
  3. News and Events

MOEVT NEWS&EVENTS

Ziara ya Muhasibu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Details
11 July 2023
240

Muhasibu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar bwana Said Seif  Said amefanya ziara na  kuzungumza na wahasibu wake wote wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na wa katiba nasheria Katika ukumbi wa Wizara ya Elimu Mazizini Unguja.

Lengo la ziara hiyo ni kuweza kujua tathmini ya mwaka wa fedha 2022-2023, kujua changamoto mbalimbali  za kazi.

Aidha amewasisitiza kufanya Kazi kwa bidii katika  mwaka mpya wa fedha 2023-2024 na kufata na sheria na  taratibu ili  kuweza kuondoa mapungufu yalojitokeza.

Utiaji Saini Makubaliano kati ya Serikali ya India na Zanzibar

Details
11 July 2023
257

NA KHAMISUU ABDALLAH

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema ufunguaji wa tawi la Chuo cha IIT Madrasa cha nchini India hapa Zanzibar utafungua fursa ya kuitangaza nchi duniani na kuwa kichocheo cha kuwavuta watu nje ya Zanzibar kujisajili katika tawi hilo kwa lengo la kupata taaluma. 

Dk. Mwinyi alieleza hayo mara baada ya kushuhudia utiaji saini makubaliano kati ya serikali ya India na Zanzibar kwa ajili ya uanzishwaji wa Chuo hicho hapa Zanzibar na uzinduzi wa website ya Chuo hicho hapa Zanzibar hafla iliyofanyika Ikulu Zanzibar.

Alisema kufunguliwa kwa tawi hilo nchini kutaleta faida mbalimbali ikiwemo Zanzibar kuzidi kujitangaza duniani sio tu kama nchi ya utalii bali ni nchi yenye Chuo kinachotambulika duniani katika fani ya Teknologia.

Read more …

Hafla ya kukabidhiana Vifaa vya Michezo kutoka Katika Jumuiya ya Zan Education and Sports Initiative (ZESI).

Details
05 July 2023
122

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa amesema  upatikanaji wa Vifaa vya kujifunzia itasaidia Sana sekta ya Elimu nchini.


Amesema hayo wakati wa hafla ya kukabidhiana Vifaa vya Michezo kutoka Katika Jumuiya ya Zan Education and Sports Initiative (ZESI) Katika viwanja vya wizara ya Elimu Mazizini Unguja.
Amesema upatikanaji wa Vifaa vya michezo hupelekea Wanafunzi kusoma kwa vitendo kitu ambacho kitaleta Ufaulu mzuri nchini.


Aidha amesema Wanafunzi kushiriki Michezo ni jambo litakalo wajenga kiafya na kuwapelekea kuepuka kushiriki katika vikundi  vya  vitendo viovu. 
Pia amewasisitiza Watendaji watakao kabidhiwa vifaa hivyo, kuhakikisha wanavitunza vizuri  vifaa hivyo ili  viweze kusaidia watoto wengi zaidi. 

Read more …

Ziara ya kukagua Miradi mbalimbali ya Ujenzi wa Skuli za Sekondari na Msingi.

Details
05 July 2023
142

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Muhamed Mussa amesema, atahakikisha anafatilia Ujenzi wa Miradi mbalimbali ya Wizara hiyo ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa Viwango imara.


Amesema hayo wakati wa Ziara ya kukagua Miradi mbalimbali ya Ujenzi wa Skuli za Sekondari na Msingi kwa Mkoa wa Mjini Magharib Unguja na Mkoa wa Kaskazini Unguja.Amesema lengo la Ziara hiyo ni kuhakikisha Miradi inapatikana na kuzinduliwa Katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar ili Wananchi wafurahie Matunda ya Mapinduzi hayo kwa kupunguza changamoto ya kupata Elimu Katika masafa mafupi.
Amesema Wakandarasi  wahakikishe wanafanya kazi mchana na usiku ili kukamilisha Ujenzi huo kama walivyokubaliana.
Aidha, Waziri Lela amesema kuwa, atahakikisha anafatilia ujenzi wa Majengo hayo ili kuhakikisha yanakamilika kwa wakati waliokubaliano.


Hata Hivyo, amewasisitiza Wasimamizi wa Majengo (ZBA) kuhakikisha wanafatilia ujenzi wa Miradi hiyo kwa kila hatua ili Majengo yakikabidhiwa yawe na Viwango Bora.
Pia amewataka Wakandarasi wa kampuni ya   Fuchs Construction Company ambao wanasimamia ujenzi wa Skuli ya chukwani ,chumbuni na Muungano kuhakikisha anaongeza bidii ili  Mirad hiyo  aweze kumaliza kwa wakati.
Kwa upande wa Ujenzi wa Skuli ya Donge na  mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja amesema, Mkandaradi wa Simba Developer anajitahidi na kuridhishwa na Maendeleo ya Miradi hiyo. 
Nae Mkandarasi wa ujenzi huo amesema, atajitahidi kuengeza kasi ya ujenzi huo ili aweze kukamilisha mapema na kulikabidhi Wizara kama walivyo kubaliana.


Kwa upande wake Mshauri elekezi ambae ni Wakala wa Majengo Zanzibar ( ZBA)  ndugu . Nahoda Mohammed Nahoda amesema , wanaendelea na Utaratibu wao wa kuhakikisha wanawasimamia wakandarasi ili kuhakikisha wanajenga kwa mijibu wa makubaliano ya kujenga majengo yenye viwango na kumakiza kwa wakati.
Katika ziara hiyo Mhe Lela alitembelea ujenzi wa Skuli ya Chukwani.Muungano, Chumbuni,Donge na MkoKotoni .

Makabidhiano ya Mtaala Mpya kwa Fani ya Biomedical Engineering Kati ya (KIST) na Ujumbe kutoka ATC.

Details
05 July 2023
120

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Abdulgulam Hussein amesema, lengo la Serikali ni kuhakikisha Elimu  ya Ufundi inapewa kipao mbele ili kuweza kuleta Maendeleo katika kila Sekta Nchini.
Amesema Hayo wakati wa Hafla ya Makabidhiano ya Mtaala Mpya kwa Fani ya Biomedical Engineering Kati ya (KIST) na Ujumbe kutoka Chuo Cha Ufundi Arusha,  iliyofanyika Katika Ukumbi wa Mikutano wa Dkt. Idrissa Muslim Hija, Mbweni Zanzibar.


Amesema, fani za Ufundi ni Miongoni mwafani ambazo zinawasaidia Vijana wengi kujiari wenyewe pasipo kutegemea ajira maofisini, jambo ambalo limewasaidia Vijana wengi kupiga hatua katika maisha yao.
Mhe. Abdulgulam amafanua kuwa, fani za Ufundi katika ngazi ya Astashahada  na Shahada  ndizo  ambazo zinasidia Vijana kujiajiri na kuajirika katika Sekta mbalimbali Nchini, hivyo uanzishwaji wa fani mpya ya Biomedical Enginnering nayo pia itatoa fursa kwa vijana kujiajiri na kuajirika Nchini.

Read more …

Page 10 of 12

  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12

Contact Details

P.O.Box 394 Mazizini, Zanzibar
+255 24 223 2827
info@moez.go.tz

Main Menu

  • Home
  • About Us
  • News and Events
  • Staff Mail
  • Contact Us

Get in Touch

P.O.Box 394 Mazizini, Zanzibar
info@moez.go.tz

Our Institute

  • Kwarara Media Education Centre (KMEC)
  • The State University of Zanzibar (SUZA)
  • Vocational Training Authority(VTA)
  • Zanzibar Higher Education Loan Board(ZHELB)
  • Karume Institute of Science and Technology(KIST)
  • Zanzibar Examination Council(ZEC)
  • Zanzibar Institute of Education(ZIE)

External Links

  • Ministry of Education, Science and Technology (MOE)
  • The National Examination Council of Tanzania (NECTA)
  • The National Council for Technical Education (NACTE)
  • Tanzania Commission for University (TCU)
© MoEVT. Designed by ICT-Department.