
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa amesema, Serikali imedhamiria kuweka mazingira bora ya elimu kwa ngazi zote ili kuleta maendeleo ya Kielimu nchini.
Ameyasema hayo wakati akifunga Maonyesho ya Nne ya wiki ya Elimu ya Juu, yaliyo fanyika katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja.
Ameseama, Maonyesho hayo ni fursa kwa wazazi na wanafunzi katika kuendelea na elimu ya Vyuo Vikuu.
Amesema, wanafunzi ni vyema kutumia fursa hiyo adhimu ya kupata kujiunga na Vyuo Vikuu kwa kwa urahisi ili kuweza kusonga mbele kielimu.
Mapema Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Khamis Abdulla Said amesema, Idadi ya Wanafunzi walofaidika kujiunga na Vyuo Vikuu kupitia Maonesho hayo ni kubwa, jambo ambalo limesaidia sana kupunguza gharama za kutafuta tarifa za Vyuo husika.