
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Muhammed Mussa amesema, Wizara Inathamini jitihada za Wadau mbali mbali katika Sekta ya Elimu ili kuleta maendeleo mazuri ya Elimu Zanzibar.
Ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa Dahali ya Kisasa ya Wanawake iliyo jengwa na Tasisi ya korea Food for the Hungry International (KFHI ) chini ya Ufadhili wa Ushirika wa Maendeleo Korea International Coperation Agency iliyoko huko Paje Mtule Wilaya ya Kusini Unguja.
Amesema, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Zanzibar imekuwa ikipokea misaada mbali mbali kutoka Kwa wadau mbali mbali ili kuweza kuboresha maendeleo ya Elimu Zanzibar.
Amesema, Wizara itaendelea kutoa mashirikiano na Wadau wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu ili kuweza kudumisha umoja na mashirikiano katika kuiboresha Sekta ya Elimu pamoja na sekta nyengine zote za kimaendeleo.